ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 27, 2011

'H BABA BURST BONGO MOVIES' BUBBLES'

Ali Kiba wa Bongo Fleva akitaka kumtoka beki wa Bongo Movie katika mechi iliyochezwa jana jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar.Bongo Fleva waibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0 yaliyotiwa kimyani na mshambuliaji H. Baba. Picha kwa hisani ya Othmani Michuzi.

Meya wa Manispaa ya Ilala Jelly Slaa akisalimiana na 'Muuaji' wa Bongo Movie H.Baba.

PICHA ZA VIKOSI KWA HISANI YA JIACHIE>Kikosi kamili cha Bongo Flava Fc.

Kikosi kamili cha Bongo Muvi Fc.

Katika matukio yaliyotengeneza historia kiwanjani hapo moja wapo ni mbwembwe za timu ya bongo Muvi wakiongozwa na kamati yao ya ufundi ikiongozwa na bi Mwenda, Mzee Chilo na wenzake. Dakika jinsi zilivyoendelea kusonga hali ilikuwa mbaya kwao kwani walionekana kukosa raha na kufadhaika mno kwa kichapo walichopokea, kama vile haitoshi mchezaji wao machachari Ben Kinyaiya ilikuwa ni kama kutia chumvi kwenye kidonda kibichi pale alipokosa penati. Dr. Mtitu wa Bongo Movie akikimbia na mpira huku beki wa Bongo Fleva akimfukuzia. Hadi mwisho Bongo Flava 2 Bongo Muvi 0. Mechi hii imefanyika kwa hisani ya kuwachangia watu waliopatwa na maafa/waathiriwa wa milipuko ya mabomu iliyotokea kambi ya Jeshi Gongo la mboto hivi majuzi.

HONGERA WASANII WA TANZANIA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.