ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 10, 2011

KILA KUKICHA .... AJALI

Kila kukicha ajali zinaripotiwa kutokea, na nyingi kati ya hizo ni ajali zinazohusisha kwa namna moja au nyingine waendesha pikipiki hii nimeishuhudia muda mchache uliopita pale dreva wa pikipiki alipokuwa akijaribu kuovateki upande wa kushoto kwenye kona finyu ya kipitashoto cha barabara ya Kenyata karibu na jengo jipya la PPF Mwanza...dreva amepata michubuko kimtindo..

Kwa Mwanza imekuwa kawaida kwa madreva wa pikipiki kujichukulia sheria mkononi pindi inapotokea mmoja wao kapatwa ajali, hawatizami nani mkosaji wanachojua ni kumwadhibu dereva wa chombo kingine kwa kumpatia kichapo au kumdhuru kwa aina yoyote ile au hata pengine kumchomea moto chombo chake cha usafiri.

Lakini pamoja na hili pia kunatukio lililoripotiwa mwishoni mwa mwaka jana desemba 23 ambapo kibao kiligeuka pale mwendesha pikipiki mmoja alipouawa na wananchi katika wilaya ya Ukerewe, Mwanza baada ya kugongana na baiskeli na kusababisha kifo cha mmoja wa watu wawili waliokuwa wakisafari kwa baiskeli hiyo.


Mwendesha pikipiki aliyeuawa alikuwa Eric Elius [34] mkazi wa kijiji cha Buhima –Ukerewe,na aliyekufa baada ya baiskeli akisafiria kugongana na pikipiki hiyo ni Matha Kanyago [20] Mkazi wa Kijiji cha Chankamba – Ukerewe na mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Igombe – Ilemela Jijini Mwanza.
TUNA KAZI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.