ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 10, 2011

SHULE ZA MSINGI ZATAKIWA KUANZISHA BENDI.

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika (mb) amezitaka kamati za shule za msingi kuhakikisha zinaansisha bendi za shule ili kuwavutia wanafunzi kupenda kuhudhuria masomo.

Uzoefu unaonyesha kuwa wanafunzi wengi wa shule za msingi hupenda kuungana na wenzao kwa mvuto wa bendi. mnamo mwaka 2002 Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ililitambulisha shirika lisilo la kiserikali la tanzania Environmental Health and Educational Services la Dar es Salaam kuwa linajishughulisha na ufufuaji wa vivutio mbalimbali vya watoto shuleni ikiwemo na usambazaji wa vifaa vya bendi vya bei nafuu.


Enzi hizo bendi ya shule ya msingi tumaini bukoba picha by Anthony Brown Masai.

Aidha, Shule za msingi hazina bendera ya Taifa katika maeneo yao. Moja katika mambo wanayofundishwa watoto ni uwepo wa Bendera ya taifa, rangi zake na maana ya rangi hizo. Wanafunzi wataelewa vizuri somo hili kwa kuiona bendera yenyewe. Wizara inasiositiza umuhimu wa shule zote kupeperusha bendera ya Taifa.

Mwisho, Ofisi ya waziri Mkuu - TAMISEMI inasisitiza kuwa michezo ni sehemu ya Elimu shuleni. Kila shule ni lazima kuwa na vifaa vya michezo na kuwashirikisha wanafunzi katika michezo. Mashindano ya michezo kwa wanafunzi katika ngazi mbalimbali yatafanyika hadi ngazi ya Taifa.

IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 09/05/2011.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.