"Nikiangalia hali ya maisha yenu wananchi wa jimbo hili, Mkoa wa Rukwa na Katavi si haki ninyi kuendelea kuishi kwenye nyumba za udongo na nyasi wakati kodi zinafujwa kila kukicha kwa matumizi ya anasa ya Serikali hii," alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alisema mbali na anasa hiyo, semina elekezi kwa mawaziri inayoendelea mkoani Dodoma imegharimu fedha nyingi na kwamba iwapo serikali ingekuwa inawajali wananchi wake, ingeweza kujenga shule za sekondari katika jimbo zima la Waziri Mkuu kwa kutumia fedha zinazotumika katika semina hiyo.
Rais akiongea wakati wa ufunguzi wa semina elekezi.
"Kikwete amewateua mawaziri kisha anawaandalia semina za kazi gani? Kama hawana uwezo wa kuongoza si angeteua wabunge wengine? Alisema mawaziri walioshindwa kufanya kazi wajiondoe wenyewe. Kwani anajua mawaziri wake hawafai, lakini badala ya kuwafukuza anawapa ruksa wajiondoe wenyewe!"
Kutoka kushoto waziri mkuu Mh.Pinda, waziri mkuu mstaafu Msuya na Mh.Rais Jk.
"Pinda, kwa siku moja akiwa kule bungeni hupata posho ya Sh200,000 ambayo inazidi mshahara wa mwezi mmoja wa mwalimu, hata polisi anayelinda usalama wenu. Lakini magari anayotumia kwenye msafara wake yasiyopungua 30 gharama yake haipungui Sh600 bilioni. Gharama ya gari analotembelea mbunge wenu ni sawa na kujenga vituo vitano vya afya."
Dk Slaa aliyekuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana alisema, inasikitisha kuona Mbunge wa Katavi anakuwa mbinafsi kwa kujiwekea umeme wa jua kwenye nyumba yake pekee katika Kijiji cha Usevya badala ya kuupeleka kwa wananchi wote.
Habari :Edwin Mjwahuzi, Mpanda na Boniface Meena Sumbawanga
Habari zaidi tembelea www.mwananchi.co.tz
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.