Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhandisi Maryprisca Mahundi, amewahimiza wanafunzi wa kike nchini kuwekeza juhudi katika masomo ya Sayansi, akisisitiza kuwa kusoma masomo hayo ni njia muhimu ya kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Naibu Waziri Mahundi ameyasema hayo leo, Februari 11, 2026, wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana Katika Sayansi, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
“Watoto wa kike, ninawaambia kusoma Sayansi inawezekana. Ukifaulu vizuri, itakuwa msaada mkubwa katika mapambano ya kujenga taifa,” amesema Naibu Waziri Mahundi.
Ameongeza kuwa jukumu kuu la wizara ni kuhakikisha wanawake na wasichana wanahamasishwa na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Sayansi, kupitia maboresho ya sera na miongozo inayowarahisishia kushiriki ipasavyo katika fursa za maendeleo ya Sayansi.
Aidha, Naibu Waziri Mahundi amesisitiza kuwa wanapowahimiza wasichana kusoma Sayansi, wizara haimuachii nyuma mtoto wa kiume, ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza za kutowapa fursa sawa watoto wa kiume katika nyanja za elimu na Sayansi.
Tupe maoni yako
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
0 comments:
Post a Comment