Hayo yamebainishwa leo Jijini Mwanza na Meneja wa Kanda ya Zanzibar, kutoka mradi wa kupambana na Malaria nchini (IRS), Bw. Abdulah Salum, wakati alipokuwa akiwasilisha mada kwenye semina ya siku tatu kuhusu athari za Malaria, iliyowashirikisha waandishi wa habari mbali mbali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, na kufanyika Midlend Hoteli jijini humo.
Amesema, ugonjwa wa malaria umekuwa tishio kwa maisha ya Watanzania, Afrika na dunia nzima, na kwamba, mradi huo wa IRS umedhamiria kupunguza kabisa mazalia ama ugonjwa huo ambao umekuwa ukiua watu wengi duniani.
Meneja huyo wa IRS Kanda ya Zanzibar, Bw. Salum amefafanua kwamba, mbali na idadi hiyo ya vifo kwa watoto, kati ya watu 80,000 wanaopoteza maisha mbali mbali, kati yake asilimia 40 wanakufa kwa ugonjwa huo wa Malaria.
Akizungumzia kuhusu vita hiyo ya kupambana na ugonjwa huo hatari, Bw. Salum ameitaja Zanzibar na viunga vyake kuwa imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kudhibiti maambukizo ya ugonjwa hatari wa Malaria, kutoka asilimia 40 mwaka 2008 hadi kufikia asilimia moja kwa sasa.
Kwa mujibu wa Meneja huyo wa IRS Kanda ya Zanzibar, Salum, upungua kwa maambukizi hayo, imetokana na mikakati thabiti ya kupambana na ugonjwa huo, hivyo Watanzania wote wanapaswa washirikiane na Serikali ukiwemo mradi wa kupambana na Malaria wa IRS ili kudhibiti kabisa ugonjwa huo.
Amewaomba Watanzania kushirikiana na mradi huo wa IRS katika kupambana na ugonjwa huo, na kwamba zoezi la kunyunyizia majumbani dawa ya ukoko linaloendelea nchini linapaswa kuungwa mkono na watu wote ili kufikia malengo ya kuwa na Tanzania siyo na malaria.Dr Pius Tubet meneja mradi wa Kanda ya ziwa Victoria akiwasilisha taarifa ya kanda.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.