Mkuu wa mkoa wa Mwanza bwana Erenest Ndikilo ofisi yake imeahidi kuunda kamati ya kuchunguza kifo cha utata cha mwandishi wa habari kanda ya ziwa marehemu Richard Masatu aliyefariki dunia mnamo tarehe 10/08/2011 nakupatikana na tundu la jeraha lililoanzia chini ya kidevu hadi kwenye koromeo.
Hayo ameyasema leo kupitia ombi lililo ambatanishwa kwenye risala yao alipotembelea Ofisi za chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mwanza (MPC) kwa lengo la kuzungumza nao. Mkuu huyo wa mkoa amewaasa wandishi waepuke kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kuchafua wenzao kwa kuandika habari zinazo poteza amani, utulivu, mshikamano na wala wasitumike kuigawa nchi kikabila, kidini na kisiasa badala yake watumie taaluma zao kushauri, kukosoa, kutoa mapendekezo na kusifu pale viongozi wanapotenda stahiki kwa jamii.
Aidha Mh. Ndikilo amewaagiza wakuu wote wa halmashauri zote za wilaya mkoani Mwanza kutoa ushirikiano kwa wanahabari ili wananchi wapate taarifa zilizo sahihi na kwa wakati.
Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wandishi wa Habari Mwanza (MPC) bi Flora Magabe akiwasilisha Risala kwa mh. mkuu wa mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo(kushoto) na aliyesimama katikati ni katibu wa MPC Edwin Soko.
Mwisho mkuu wa mkoa amewasihi wandishi wa habari kuwa na utaratibu wa kufika sehemu za vijijini kukusanya habari , taarifa na matukio kwa lengo la kuikwamua jamii hiyo muhimu.
WAZIRI MKUU AZINDUA ALBINO MOBILE APP
-
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
amezindua 'Albino Mobile App' ambayo ni program ya simu janja
itakayowezasha usajili na...
GEORGE MASAJU ATEULIWA JAJI MKUU
-
*Na Happiness Katabazi.*
*RAIS Samia Suluhu Hassan Leo amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani George
Mcheche Masaju Kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.*
*Kwa Mujibu ...
TAZAMA USIKU WA BI FELISIA KYAMANI ULIVYO FANA
-
Wanafamilia na Waalikwa wakicheza kwaifuraha na shangwe kwenye siku hii
muhimu ya SendOff ya Bi Felias Kyamani .
Watu walivaa na kupendeza Ukumbi ulipambw...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.