ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 1, 2011

MEI MOSI 2011, WAFANYAKAZI BADO HAWANA CHA KUJIVUNIA.

Mmoja wa wafanyakazi ambaye jina lake halikuweza kufahamika akiwa bize na kufuma kitambaa viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambazo kitaifa zimefanyika mkoani Morogoro.

Wakati leo wafanyakazi nchini Tanzania wamejumuika na wafanyakazi wenzao duniani kuadhimisha siku ya wafanyakazi ulimwenguni ijulikanayo kama MEI MOSI na hapa nchini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akihudhuria kama mgeni rasmi kwenye sherehe hizo zilizofanyika kitaifa mkoani Morogoro hali bado si hali katika haya:-

Mishahara duni, kukatwa kodi kubwa, gharama za maisha kuongezeka, mazingira magumu ya kazi na mafao kiduchu ya uzeeni ni mambo yanayopunguza ari ya kazi!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.