Meneja wa mauzo na usambazaji TBL kanda ya ziwa Malaki Sitaki (aliyesimama), pembeni yake ni Special Event Manager wa kampuni hiyo Erick Mwayela na mwisho kabisa ni Katibu tawala mkoa wa Mwanza Bi. Dorothy Mwanyika. Jumla ya timu 23 za mikoa mbalimbali hapa nchini zimepangwa kushiriki michuano ya Kili Taifa Cup 2011 kwa makundi sita ambapo kila mkoa umetengewa fungu lake kwa ajili ya maandalizi ya awali.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mchango huo na kisha kuuwasilisha papo hapo kwa mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mwanza (MZFA) Jackson Songora, mkuu wa mkoa wa Mwanza Abass Kandoro amesema ofisi yake itatoa shilingi milioni moja kuchangia maandalizi hayo ambapo mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 3.8 zinahitajika kwenye bajeti ya shilingi milioni 7 iliyowekwa.
Pia mkuu huyo ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo, mashirika binafsi na wafanyabiashara wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kuisaidia timu hiyo ili ishiriki vyema kwenye mashindano hayo na hatimaye ipate ushindi.
Awali mashindano hayo soka ya Taifa Cup ndani ya TBL yalikuwa yakidhaminiwa na bia ya Safari Lager ambapo kampuni hiyo baadae katika maamuzi yake na sababu maalum iliamua kuhamisha udhamini wa michuano hiyo kwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.