ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 29, 2011

FILAMU YA MAUAJI YA ALBINO YAZINDULIWA.

Filamu ya mauaji ya waafrika wenye ulemavu wa ngozi imezinduliwa rasmi jana katika ukumbi wa Nyumbani Hotel jijini Mwanza .Ni filamu iliyo katika muundo wa makala imetengenezwa kwa lengo la kuelimisha jamii kuziepuka mila potofu kwamba viungo vya albino ni dawa ya bahati sambamba na kupaza sauti kufichua ubaguzi uliopo juu ya watu wenye ulemavu huo.

Rais wa shirika la kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi linalofahamika kwa jina la UNDER THE SAME SUN, Peter Ash akiwa na mratibu wa shirika hilo hapa nchini Vick Ntetema wakizungumza na wadau toka makundi mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari walioalikwa kwenye kusanyiko hilo la kuitambulisha filamu hiyo sambamba na kuijadili elimu itokayo filamuni.

Mwenyekiti wa chama cha wenye ulemavu wa ngozi mkoani Mwanza akizungumza wakati wa ufanguzi wa kusanyiko hilo.

Kupitia mauaji ya albino yaliyozuka hivi karibuni na kuumiza ulimwengu, familia nyingi zimepoteza watoto wao na ndugu zao, mfano hai ni Babu na bibi Letisia (kushoto) wa kijiji cha Kashindaga ambao walimpoteza mjukuu wao aitwae Letisia, kulia ni Mama Manyashi na mumewe wa sasa ambaye mtoto wake aliuawa kwa kukatwa mapanga baada ya mumewe wa awali kushiriki kutimiza mauaji hayo kwa kulipwa kiasi cha shilingi laki mbili ili wauaji wachukuwe viungo vya mwanae Yunis.

Sehemu ya filamu hiyo ikimuonyesha babu yake Letisia akielekeza mahala alipomzika mjukuu wake chini ya kitanda chake, na amefanya hivyo kwani kulikuwa na mtindo wa watu kufukuwa makaburi ya albino na kuchukuwa viongo.

Katika sakata hili linalohusisha imani za kishirikina nao waganga wakienyeji wakitajwa kuwa ni kichocheo kikubwa, ni wengi wamepoteza maisha yao na wengi wamenusurika huku wengine wakibakiwa na ulemavu wa kudumu na makovu yasiyoisha.

Sehemu ya filamu...
"Tunataka mauaji yakomeshwe na haki itendeke kwa wavulana na wasichana waliopoteza maisha yao kwa kuchinjwa kinyama"

Mkutano ukiendelea.

M-blogishaji maarufu nchini kupitia blogu ya MTAA KWA MTAA anaitwa Othman Michuzi akihusika kikamilifu kupasha habari kwa umma kupitia mtandao wake.

Elimu ipanuliwe kwa watu, kisha akatumia na mistari ya biblia soma Yohana 10:10, Mathayo 11:28. Mwanachuo kutoka chuo cha SAUTI Mwanza Monalisa Juma wakati akichangia mawazo mara baada ya kuiona filamu.

Wakuu wa vikundi vya dini mbalimbali nao walikuwa sehemu ya waalikwa.

Picha ya pamoja nami.
Filamu hii imehusisha zaidi watu ambao maelezo yao ni ushuhuda wa ujasiri na ukakamavu wa mwanadamu ambaye anatumika kupaza sauti na kufichua undani wa yale maovu yanayotendeka kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.