Bi. Mwanyika ameiasa jamii kuepuka vitendo vyote vinavyochangia kwa kasi uzalishwaji wa kemikali hizo zenye madhara kwa binadamu ambazo husababisha maradhi kama saratani katika maeneo mbalimbali mwilini mabadiliko katika mfumo wa kinga na madhara katika mfumo wa fahamu.
Polychlorinated dibenzo-p-dioxins (PCDD) kwa kifupi dioxin na polychrinated dibenzofurans (PCDF) kwa kifupi furans ni kemikali mbili miongoni mwa kemikali 12 zinazochukua muda mrefu kutoweka katika mazingira ambazo zinathibitiwa kwa lengo la kulinda afya ya binadamu.
Kemikali hizi huzalishwa bila kukusudia wakati wa mchakato wa shughuli za uzalishaji bidhaa viwandani na uchomaji taka. Shughuli nyingine ambazo zimetajwa kama sehemu ya uzalishaji sumu hatari kwa afya ya binadamu ni pamoja na uchomaji taka za hospitali kwa kutumia mitambo isiyo bora, uzalishaji wa bati na chuma, uzalishaji wa saruji, chokaa, matofali na vioo, mitambo ya kuzalisha nishati inayotumia mafuta, kuni au mabaki mengine ya wanyama na mimea.
Kwa upande wake ameiasa Jamii kuepuka kuchoma taka ngumu hata zile zenye dutu za sumu au kuwasha jiko la mkaa kwa kutumia bidhaa za plastiki na kwa wale wenye viwanda amewataka kujiunga na teknolijia bora zilizopo za utunzaji mazingira kwa kuzingatia miongozo iliyoandaliwa na Sekretarieti ya mkataba wa Stokholm ambapo serikali imedhamiria kuifikisha kwa kila kiwanda.
Mipango kudhibiti imeundwa kubaini na kudhibiti uzalishaji wa kemikali hatarishi kwa mazingira kwa kutoa elimu ya madhara ya sumu hiyo hatari sambamba na kukuza upatikanaji wa njia mbadala wa kuzuia uteketezaji wa taka ngumu.
kwa msaada zaidi angalia tovuti www.pops.int
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.