ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 26, 2018

WATANZANIA BADO TUKO NYUMA SUALA LA UTALII WA NDANI.

 NA.MANDIA ZEPHANIA MWANZA
Watanzania wametakiwa kutambua umuhimu wa utalii wa ndani kwa kujenga desturi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza uelewa wa maswala mbalimbali pamoja na kujionea vivutio mbaimbali katika hifadhi hizo.

Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Kisiwa cha Utalii Saa Nane BEATRICE KESSY amesema hifadhi hiyo imelenga kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo kutoka elfu kumi kwa mwaka hadi kufikia elfu kumi na tatu kwa mwaka kupitia kampeni ya GUDUA HAZINA ZA UTALII MWANZA inayohamasisha wanafunzi kutembelea hifadhi hiyo.


Hifadhi ya taifa ya Saa nane ni hifadhi pekee iliyopo katikati ya jiji la Mwanza ikiwa ni hifadhi pekee iliyopo katikati ya jiji yenye vivutio mbalimbali ikiwemo wanyama  na manthari ya kuvutia.

Mhifadhi mkuu wa hifadhi hiyo BEATRICE KESSY amesema kuanzishwa kwa kampeni ya GUDUA HAZINA ZA UTALII MWANZA, imejikita kuhamasisha utalii wa ndani pamoja na kuongeza idadi ya watalii katika hifadhi hiyo.

GLORIA MWIHAMBO msimamizi wa bodi ya utalii kanda ya ziwa (TTB),amesema ukilinganisha na miaka iliyopita watanzania wamepata muamko wa  kutembelea hifadhi mbalimbali nchini.

Watalii kutoka hao kutoka vyuo mbalimbali vya mkoa wa Mwanza wamesema imekuwa fursa kwa wao kuongeza uelewa katika masomo yao pamoja na kufurahi vivutio mbalimbali katika hifadhi hiyo.

Hifadhi hiyo iliyopo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) limeanzisha kampeni hiyo itakayodumu kwa siku tatu ambapo pamoja na kutembelea hifadhi hiyo wanafunzi hao watashiriki michezo mbalimbali pamoja na kutoa zawadi kwa mwanafunzi  atakaye  tangaza hifadhi hiyo vyema kupitia mitandao ya kijamii.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.