ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 26, 2018

KAULI YA MATAKA BAADA YA KUJIENGUA ALLIANCE.

KOCHA Mkuu wa timu ya Alliance FC ya Mwanza, Mbwana Makata, amesema kuingiliwa majukumu yake ni moja ya sababu iliyomfanya kujiweka pembeni kwenye kikosi cha timu hiyo.

Makata pamoja na msaidiziwake Renatus Shija, hawakuwepo kwenye benchi wakati timu hiyo ilipokuwa ikiumana na Simba kwenye Uwanja wa taifa Dar es Salaam na kukumbana na kipigo cha mabao 5-1.

Alisema imefikia hatua yeye kama kocha hana mamlaka ya kupanga kikosi na kuingiliwa na menejimenti ya timu hiyo.

“"Suala la mchezaji gani anastahili kucheza na mwenye jukumu la kupanga na kufundisha  kikosi ni mwalimu, hivyo unapoingiliwa kwenye majukumu unaonekana kama hufai  na unaharibu taaluma hivyo kufuatia hilo nikaamua kujiengua na ndicho kilichotokea katika mchezo wetu dhidi ya Simba," alisema Makata.

Alisema, Meneja wa timu kimsingi anapaswa kukaa nje ya benchi la ufundi na kushuhudia nini timu yake inafanya  hivyo suala ya kuingilia katika kupanga kikosi siyo jambo jema na mwenye jukumu hilo ni kocha mkuu wa timu pamoja na msaidizi wake.

Makata, alisema kwa sasa wanasubiri hatima yao kutoka kwa menejimenti ya timu hiyo lakini alisisitiza hayupo tayari kufanya kazi kwa kupangiwa na watu ambao hawana taaluma ya ukocha.

Kwa upande wake Meneja wa timu hiyo FC, James Bwire, ambaye anashutumiwa kumuingilia kocha huyo, alisema suala la yeye kuhitafiliana na makocha wake ni jambo geni, kwani yeye kama meneja anatambua majukumu pamoja na mipaka yake hivyo na wao watambue pia.

Bwire alisema hoja ya sasa siyo kutofautiana kimsingi ni kutafuta njia mbadala ya namna ya kusaidia timu kupata matokeo mazuri hayo.

Alisema tuhuma hizo zinazoelekezwa kwake ni kisingizio kwa kuwa mpaka sasa kocha huyo (Makata )amehamisha kila kitu  kwenye nyumba waliompangia.

"Mpango wa kuhama alikuwa nao, hivyo tulimpa mechi mbili za Simba na Yanga kuwa hakipoteza safari yake na timu hiyo itakuwa imeishia hapo, ila yeye amejiwai kuondoka kwa kisingizio cha kuingiliwa majukumu yake, kavunja mkataba mwenyewe hivyo taratibu za kulipwa stahiki zake zitafuatwa kama sheria inavyo elekeza, hata kama kunatofauti kati yetu angesubilia mchezo upite kwanza baada ya hapo tungekaa pamoja kujadiliana lakini yeye akaamua kuitelekeza timu. ", alisema Bwire.

Alliance iliyopanda daraja msimu huu, inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi sita baada ya kucheza michezo 11.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.