Airtel yatangaza washindi wa shindano la video bora lijulikanalo kama “Jicho la Kitaa”
· Washindi wawili wapatikana kila mmoja kajishindia shilingi millioni tano na nafasi ya kwenda kwenye mashindano ya kimataifa nchini Singapore
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza washindi wawili wa shindano la Jicho la kitaa lililokuwa likiendeshwa kupitia mitandao yake ya kijamii ya faceebook na Instagram na kuwapa nafasi watanzania wenye vipaji vya kutengeneza filamu ya dakika 5 yenye maudhui ya connecting life yaani kuunganisha jamii kushiriki na kujishindia zawadi nono.
Akitangaza washindi wa jicho la kitaa, Jaji wa shindano hilo na mmiliki na mkurugenzi mkuu wa studio ya picha ya I-View, Raqey Mohamed alisema “ shindano la jicho la kitaa limekuwa na ushindani mkubwa, zaidi ya filamu fupi 120 zimetumwa na tumezipigia zote na hatimae kupata washindi wawili . napenda kuwapongeza sana kwa kazi zao nzuri kwa maani huu ndio mwanzo mzuri wa kuinua kazi zao na kuzifikia ndoto zao
Raque aliwataja washindi hao na kusema “ninayofuraha kutangaza washindi wetu ambao ni Santos Hillary mwenye filamu yake ijulikanayo kama “ uliza kiatu “ na mshindi wa pili ni Elly EMD filamu yake inaitwa “Day by Day” nawapongeza sana washindi wetu na wote walioshiriki.”
Kwa upande wake Afisa uhusiano wa Airtel , Bi Jane Matinde alisema “ kila mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 5 pesa taslimu pamoja na kupata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa yanayotegemea kufanyika tarehe 21 mwenzi huu nchni Singapore.
Nawashukuru vijana wenye vipaji walioshiriki katika shindano hili na kuwahasa kuendelea kuchangamkia fursa kama hizi kupitia program zetu mbalimbali kwani ndio mwanzo mzuri wa kuinua vipaji vyao na kuzifikia ndoto zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.