Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, (jina lake halikufahamika mara moja) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa ameokotwa majira ya saa tano asubuhi jana akiwa amekufa na mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la mpunga nje kidogo ya eneo la chuo hicho.
Mbali na kuthibitisha kifo hicho, kiongozi huyo ameeleza pia kuwa, msichana huyo ni mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila hakuwa mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai.
Ameongeza pia kuwa, msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa walimu wa Sanaa chuoni hapo.
Taarifa za awali zilieleza kwamba usiku wa kuamkia tarehe 2 Novemba, Juliana alikwenda kwenye “birthday party” katika Lodge moja maeneo ya mkabala na Chuo cha Tumaini Makumira pembezoni mwa barabara ya Moshi – Arusha, lakini asubuhi yake mwili wake ndipo ukakutwa katika mashamba hayo ya mpunga ambayo yapo kati ya barabara hiyo ya Moshi – Arusha na lodge ambayo birthday hiyo ilifanyika. Chini ni picha mbalimbali za Juliana enzi za uhai wake.
Juliana na hisia kutoka moyoni.
Ameongeza pia kuwa, msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa walimu wa Sanaa chuoni hapo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.