ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 19, 2012

BRIGEDIA JENERALI MWAKANJUKI AFARIKI DUNIA

Alipotembelewa na waziri Mkuu Mh. Pinda kujuliwa hali enzi zake za uhai wake Brigedia Jenerali mstaafu Mwakanjuki (kulia).
Waziri wa zamani katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Brg. Gen. Mstaafu Mwakanjuki amefariki dunia mchana wa leo ktk hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es salaam.

HISTORIA yake inaonyesha kuwa miaka ya nyuma Jenerali huyo alikuwa askari polisi katika serikali ya Kibaraka wa Waingereza na Waarabu akiwa ndo kwanza kijana yaani PC katika kituo kikuu cha Malindi, Yeye pamoja na wananchi wengine hawakuufurahia uhuru feki wa Zanzibari kabla ya mapinduzi.

Amekuwa Waziri, Mbunge na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi wa muda mrefu anamwelezea marehemu kuwa.. Isingekuwa maamuzi mazuri ya Mwakanjuki katika siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, mapinduzi hayo yasingeweza kutokea au labda yangetokea kwa shida shida na huenda Wazinzibari wengi wangechinjwa vibaya sana siku hizo.

Jumbe alisema Mwakanjuki alikuwa zamu katika ghala la kutunzia silaha la polisi siku ya mapinduzi, na alipoona wananchi walioiasi serikali ya KiSultani wanakikaribia kituo chake ili wakiteke, badala ya kujihami kama ilivyo kwa askari yeyote mtiifu, lakini yeye akafungua ghala hilo na kuanza kugawia wananchi silaha na huo ndo ukawa mwanzo mpambano mkali kati ya jeshi la sultani na wananchi na hatimaye kupatikana kwa Mapinduzi hayo na Kukimbia kwa Sultani.

Hiyo ndiyo sababu watawala wengi huko Zanzibar kwa nyakati tofauti mpaka ule wa Amani Karume, hawakuweza kumsahau Mwakanjuki,bali walikuwa wakimpa titles tofauti tofauti, mara Mbunge wa kuteuliwa na Waziri, mara wa Kilimo, mara Uchukuzi etc almradi tu anakuwepo katika baraza la mawaziri akiwa Mkristo peke yake!.

Nakumbuka alipata ajali mwaka juzi vile akitokea Dodoma kwenye Halmashauri Kuu ya CCM na hali yake iliendelea kusuasua mpaka umauti ulipomfika.
MWENYEZI MUNGU TWAKUOMBA UILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMEN.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.