ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 18, 2012

TOTO YAENDELEA KUGAWA DOZI ZA JIONI YAMNYWESHA AFRICAN LYON DAWA 3 CHUNGU

Kikosi cha Toto Africans 2012.
Mara baada ya kutembeza kichapo cha 3-2 kwa Yanga mwishoni mwa wiki Toto Africans ya jijini Mwanza leo tena imeendeleza wimbi lake la kugawa dozi za jioni ikijitengenezea mazingira mazuri kuukwepa mstari wa hatari wa kushuka daraja mara baada ya kuizabua African Lyon ya jijini Dar es salaam bao 3-0 katika dimba lake la CCM Kirumba Mwanza.
Madaktari wa wakimpatia tiba beki wa Toto Africans aliyeumia kwenye paji la uso na kuvuja damu nyingi mara baada ya kugongana na mchezaji wa Lyon.
Wakiliandama lango la Lyon na kucheza kufa na kupona Toto walianza mbio zao za kuusaka ushindi kwa goli safi la dakika ya 12 mfungaji akiwa Mussa Said Mussa aliyepokea pande safi toka kwa winga aliyekuwa akihaha uwanja mzima Emma Swita.

Mara baada ya bao hilo African Lyon ilirejea kwenye mchezo lakini mashuti ya wachezaji wake Hassan Goboso na Benedict Jackob hayakuwa na macho kuziona nyavu za Wanakishamapanda.

Wakati wapenzi wa kandanda wakiamini kuwa kipindi cha kwanza kitayeyuka kwa matokeo yaleyale ilikuwa ni dakika ya 43 Iddy Moby aliyeitumia vyema pasi ya Mnaigeria Enyina Darlington kwa kuipatia Toto goli la pili. Hadi mapumziko Toto ilikuwa inaongoza goli 2 - 0.

Kasi ya mchezo ilirejea upya kipindi cha pili kwa pande zote mbili kushambuliana na kucheza kandanda salfi la kuonana. Hatimaye mwiba wa mwisho kwenye jeraha la Africa Lyon ukashindiliwa na Salum Kamana aliyefunga katika dakika ya 87 ya mchezo.

Hadi Mwisho wa game Toto 3 African Lyon 0.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.