Drogba alifunga katika kipindi cha kwanza, baada ya dakika mbili kuongezwa, huku vijana wa meneja wa Chelsea, Roberto di Matteo wakiimarisha ngome kali katika uwanja wao wa Stamford Bridge.
Barcelona waliumiliki mpira daima katika mechi hiyo, lakini walishindwa kumpita kipa wa Chelsea, Peter Cech.
Mara mbili Barcelona waligonga mwamba, lakini kweli bahati haikuwa yao. Hayo yalimpata Alexis Sanchez katika kipindi cha kwanza, na baadaye naye Pedro akitumaini kufunga bao la chini kwa chini, hakufanikiwa, na baadaye mkwaju wake pia ukigonga mwamba.
Kiungo cha kati wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas, naye alielekea kufunga, lakini mpira ukaokolewa na Ashley Cole kabla tu ya kuingia wavuni.
Ingawa Chelsea imefanikiwa kuongoza mkondo wa kwanza wa nusu fainali baada ya timu hizo kukutana Jumatano jioni, bila shaka wachezaji hao wa timu ya England wanafahamu watakuwa na kibarua kigumu katika uwanja wa Nou Camp wiki ijayo katika mkondo wa pili.
CHANZO: bbc swahili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.