ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 18, 2012

TUMENUIA KUUKUZA UTALII WA MWANZA

Mtaalam wa Masuala ya Utalii wa Tanzania kutoka TPSF Mary Kalikawe akiwasilisha vivutio alivyoviona mkoani Mwanza.
Mkutano wa kujadili ukuzaji wa Shughuli za Utalii hapa nchini umefanyika mkoani Mwanza katika ukumbi wa mikutano Gold Crest ukiwa na malengo ya kutambulisha rasilimali za kitalii zilizopo Kanda ya ziwa ikiwa ni pamoja na kujadili juu ya kutambulisha utalii uliopo Mwanza, kuutanua utalii na kuzijadili changamoto za utalii zinazopaswa kuboreshwa.

Lengo kuu la ni Kuuelezea Umma na Ulimwengu mzima kwamba kuna njia mbadala rahisi kuifikia Mbuga ya Serengeti kupitia Mwanza, na katika hilo wameshirikishwa wadau mbalimbali toka mikoa inayojishughulisha na shughuli za kitalii nchini kama waongoza utalii, pamoja na watalii walioalikwa kuona uwekezaji uliopo Mwanza na umahiri wa Mwanza ili kuiuza Mwanza katika soko la utalii, hivyo wamekusanyika hapa kujadili masuala waliyojifunza kuhusu utalii wa Mwanza sambamba na kuainisha maboresho.

Kutoka kushoto Joseph Laurent (Mkurugenzi Mwanza Guide Online Ltd ambaye pia ni Katibu wa Mwanza Tourism Association), Mary Kalikawe (Tourism Specialist) na Junaid Kadr (Co. Founder and Chairman Tanzania Developement Initiative)
Jiji la Mwanza kwa sasa lina makampuni ya kuongoza watalii yapatayo 28 ambao hufanya shughuli za kuongoza watalii ambao huja kujionea Mbuga za utalii zilizopo katika visiwa vya Ziwa Victoria, Hali ya hewa isiyo joto wala isiyo baridi, Vivutio vya Utamaduni na Historia vilivyopo jijini Mwanza pia ukaribu wa kuelekea mbuga ya Serengeti iliyopo mkoani Mara.

Wawakilishi sekta ya utalii kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Changamoto kuu zinazoukabiri mkoa wa Mwanza ni pamoja na kutokuwepo uwanja wa ndege wa kimataifa pamoja na Mkoa bado haujachagua utalii wa Mwanza uongozwe na kitu gani.

Kutoka kulia ni Charles Lupilya ambaye ni Afisa Mkuu Mtendaji Bodi ya Utalii Dar es salaam, anayefuata ni Emmanuel Mussimo (Afisa utalii mkoa wa Mara), Junaid Kadr (Co. Founder anda Chairman TDI), na Mary Kalikawe (Tourism Specialist),

Jiji la Mwanza tayari limejizatiti katika suala zima la mahoteli.
Ili kuufikia utalii mkoani Mwanza ni Nchi zilizo karibu tu ndizo hutumia usafiri wa njia ya barabara ambazo ni Rwanda, Burundi pamoja na wageni watokao uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi nchini Kenya.

Taswira ya engo ya Mkutano huo na wadau wake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.