ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 25, 2015

HAKIELIMU YAZINDUA JOPO LA WASHAURI MABINGWA

Timu ya Menejimenti ya HakiElimu ikiwa katika picha na Mwenyekiti wa Bodi ya HakiElimu na Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa jopo la washauri bingwa
Wafanyakazi wa Shirika la HakiElimu waliohudhuria uzinduzi katika picha ya pamoja na jopo la washauri bingwa
Waliosimama ni Prof. J. Galabawa (kushoto) Prof. Kitila Mkumbo (katikati) na Prof. Elias Jengo (kulia) Waliokaa ni John Kalage (Mkurugenzi wa HakiElimu) Prof. G.Mmari (katikati) na Prof. Prof. Martha Qorro (Kulia).
Mgeni rasmi Prof. Geofrey Mmari,akizungumza jambo katika hafla fupi ya uzinduzi wa jopo la washauri mabingwa akitoa neno la ufunguzi.
Prof. Kitila Mkumbo mmoja wa wajumbe wa ThinkTank akitoa neno kwa niaba ya jopo la washauri bingwa wa HakiElimu.
Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu Bi, Joyce Sekimanga kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiwasilisha ujumbe kutoka serikali katika uzinduzi wa jopo la washauri wa HakiElimu
Prof. Martha Qorro mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu kutoka kwa mgeni Rasmi Prof Geofrey Mmari
Prof. J. Galabawa mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu John Kalage akielezea lengo la kuanzishwa kwa Think Tank
Washiriki katika uzinduzi wa jopo la washauri mabingwa wa HakiElimu





Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SHIRIKA la HakiElimu  limezindua Jopo la Washauri Mabingwa  linaloundwa na maprofesa 10 waliobobea katika fani ya elimu ili  kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa watoto kupata elimu bora.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu , John Kalage amesema kazi ya jopo hilo itakuwa kutoa ushauri wa kitaalam juu ya masuala ya elimu kadri litakavyoombwa na  HakiElimu.

Amesema jopo hilo litatatoa ushaufri juu ya mikakati ,taratibu na mbinu za kuhakikisha ushiriki madhubuti katika kukuza na kutetea ubora wa elimu nchini.

Kalage aliwataja maprofesa wanaounda jopo hilo kuwa ni Abel Ishumi,Herme Mosha,Justinian Galabawa,Kitila Mkumbo,Suleiman Sumra,Martha  Qorro, Mwajabu Possi,Akundaeli Mbise, Masalukulangwa pamoja na Elias Jengo.

Amesema kuanzishwa kwa jopo hilo litasaidia shirika kupata mawazo mapana zaidi ya kitafiti na uchambuzi wa changamoto za sekta ya elimu.

Kalage amesema kuwa jopo hilo litakwenda sambamba na jitihada za serikali kuwa na mikakati mingi ya kuboresha elimu na azma ya serikali kutekeleza maazimio mbalimbali ya kimataifa kama  Malengo Maendeleo Endelevu (SDGs)na Incheon ya uboreshaji wa elimu.

 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.