ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 27, 2015

KITUO CHA KILIMO N AUFUGAJI KUJENGWA WILAYANI KIBAHA KUUNGA JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA SEKTA YA KILIMO.

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza sekta ya kilimo Chama cha wakinamama wataalamu katika sekta za kilimo mifugo  pamoja na mazingira Tanzania (TAWLAE) wamejiwekea mikakati ya kujenga kituo maalumu  cha kilimo na ufugaji  katika kata ya Pangani iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa TAWLE Dr. Sophia Mlote katika ufunguzi wa  mkutano wa siku tatu  uliowakutanisha wadau mbali mbali wa maendelea  pamoja na wataalamu katika sekta ya kilimo na ugugaji kwa lengo la kuweza kujadili changamoto zilizopo pamoja na kuweka mpango mkakati wa kuimarisha kilimo cha kisasa pamoja na ufugaji.

Dr.Sophia alisema kwamba nia wameamua kukutana wataalamu  wa kilimo na mazingira ili kuweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo sambamba na kujenga kituo hicho maalumu ambacho kitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi  wa Wilaya ya Kibaha  na Taifa kwa ujumla kutokana na kituo hicho kitakuwa kinajihusisha na kutoa mafunzo  ya kilimo pamoja na masuala mbali mbali ya ufugaji.

“kitu kikubwa katika mkutano wetu huu ambao umeshirikisha wakinamama ambao ni wataalamu katika sekta ya kilimo, mazingira pamoja na uvuvi ni kujadili masuala mabli mbali ambayo yanayohusiana na utafiti ya kilimo ili kuweza kuweka mipango mizuri ambayo itaweza kuleta mabadiliko chanya katika kuwasaidia wakinamama kupitia kilimo,”alisema Dr Sophia.

Aidha alisema kwamba kwa sasa tayari wameshapata eneo kwa ajili ya kujenga kituo hicho katika Wilaya ya Kibaha ambacho maandalizi yake yameshaanza kufayika na kwamba hati imepatikana hivyo ana imani kukamilika kwa kituo hicho cha kilimo na ufugaji kitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kibaha na maeneo mengine.

Kwa upande  wake Katibu mkuu mtendaji wa  jukwaa la wadau wa sekta ya kilimo linaloitwa (ANSAF) Audax Rukonge amesema kuwa sekta ya kilimo pamoja na mazingira ina umuhimu mkubwa katika jamii inayotuzunguka ya watanzania hivyo serikali inapaswa kutilia mkazo suala hilo kuanzia ngazi zote za kuanzia uzalishaji mpka hatua ya utunzaji  wa chakula.
Awali akitoa hotuba yake wakati alipokuwa anafungua mkutano huo katibu mku u wa Wizara ya maendeleo ya mifugo  na uvuvi  Dr.Yohana Budeba amesema kwamba serikali itahakikisha inapambana vilivyo katika kuboresha sekta ya kilimo, mifugo pamoja na uvuvi ili kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kupata ajira na kuondokana na janga la umasikini.

Katibu huyo mkuu alisema kwamba anatambua kilimo katika nchi ya Tanzania kina umuhimu sana hivyo atahakikisha anashirikina bega kwa bega na wakinamama hao ili waweze kutimiz amalengo waliyojiwekea katika kuendeleza kufanya utafiti wa kina katika mambo mbai mbali amabyo yataweza kuwasaidia wananchi katika upatikanaji wa ajira.

Katika hatua nyingine Katibu huyo alisema alengo kubwa la serikali ni kuweka utaratibu mzuri wa kuwajengea uwezo  watumishi wa umma pamoja na vikundi mbali mbali katika ili kuvipa ujuzi ambao utaweza kuisaidia sekta hiyo ya kilimo kutokana na mafunzo mbali mbali ambayo yatakuwa yanatolewa.

 MKUTANO huo   wa 19 kufanyika kwa wakinamama hao umefadhiliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Agriculture non state Actor forum (ANSAF)limewashirikisha washiriki zaidi ya 100  ambao ni wataalamu  katika sekta ya  kilimo, pamoja na mazingira kwa lengo la kujadili masuala mbali mbali ambayo yataweza kusaidia kuleta mabadiliko makubwa  hususan kwa wakinamama  kuweza kujikwamua  kiuchumi bila ya kuwa tegemezi pamoja na kutengeneza ajira kwa watu mbali mbali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.