ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 22, 2015

WAJASILIAMALI WA RUZUKU ZA SAFARI LAGER MWANZA WAPEWA MAFUNZO

 Mtaalam muelekezi wa Biashara kutoka TAPBDS Masubi B. Kandoro akifafanua jambo kwa wajasiliamali wanaopewa mafunzo maalumu ya ujasiliamali yaliyofanyika kuanzia Aprili 13,2015 na kumalizika April 17,2015 katika hoteli ya Starmax jijini Mwanza.  
LENGO NA MANUFAA YA CHANGAMOTO MSIKILIZE MTAALAMU. 

Mshauri wa biashara kutoka TAPBDS Theresia Kato alifafanua kuwa, baada ya mafunzo hayo patafuatiwa na makabidhiano ya vifaa vyao walivyoomba kwa nyakati tofauti ambapo;
 Baadhi ya washiriki hao kwa mkoa wa Mwanza wakiwa darasani wakati wa kupatiwa mafunzo.
 Darasa linaponoga.
Mshauri wa biashara kutoka TAPBDS Theresia Kato akipitia wakufunzi wake kuona utendaji wao.
Happiness Mabula Mandula ambaye ni mbunifu wa mavazi sambamba na utengenezaji batiki anaamini kuwa kupitia Safari wezeshwa biashara yake itakuwa. BOFYA PLAY.

Jemes Edward Mwandefu mjasiliamali kutoka Bariadi anajishughulisha na utoaji wa huduma za Sekretari. BOFYA PLAY.

Khadija Liganga mbunifu wa mavazi na fundi wa nguo za vitenge mafunzo yamembadilisha, wafanyabia shara wengi wanawekeza katika ubora wakisahau kujitangaza na kusaka masoko. BOFYA PLAY.

Zebedayo Lazaro Kingi mjasiliamali kutoka Bariadi anasema mahusiano ndiyo silaha, jeh ni kipi kingine alichojifunza? BOFYA PLAY

Majina ya wajasiliamali waliofuzu kupewa ruzuku za programu ya Safari  Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa mkoa wa Mwanza ni kama ifuatavyo kwenye orodha.
MWANZA
1.Bagaile Shaban Barabara
2.Dastan Mutayoba Amon
3.David Awasi
4.Godlove Charles Muro
5.Happiness Mabula Mandula
6.Jemes Edward Mwandefu
7.Khadija Liganga
8.Raymond Emmanuel Kamisha
9.Zebedayo Lazaro Kingi
10. Zeda Lucas Magomola

Mafunzo yanayotolewa ni chachu kwa biashara zao na kwa wafanya biashara wengine wanao wazunguka kwani licha ya kuwawezesha katika suala la mitaji na vitendea kazi pia yamelenga katika kuwakuza kielimu kujua jinsi ya kuboresha bidhaa zao, utanuzi na usakaji masoko.

Zoezi hili la utoaji mafunzo limehusisha wataalamu wenye uwezo na uzoefu mkubwa katika kushauri na kusaidia ukuzaji wa sekta ya biashara ndogo dogo na kubwa.

Kabla ya washiriki kupatikana toka mikoa mbalimbali nchini mchakato ambao ulikuwa mzito, jumla ya fomu za maombi zilizoifikia kamati toka mikoa yote shiriki nchini zilikuwa ni 3,613.  Wajasiliamali walifuzu vigezo ni 55 kutoka kanda tatu tofauti. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.