ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 25, 2015

MIKOA MITANO KUSHIRIKI DARTS TAIFA.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakipasha kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yaliyofunguliwa jana Moshi Hoteli Manzese jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakipasha kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yaliyofunguliwa jana Moshi Hoteli Manzese jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es Salaam.
Mikoa mitano kushiriki Darts Taifa
Na Mwandishi Wetu.
MASHINDANO ya mchezo wa Darts Taifa yamezinduliwa jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Moshi iliyopo Manzese kwa kushirikisha mikoa mitano ya Tanzania.

Akizindua mashindano hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya kinondoni, Selestine Onditi ”kwanza aliwapongeza viongozi wa chama hicho kwa juhudi za pekee za kufanya mashindano hayo yafanyike kwa mwaka wa 2015,lakini zaidi aliwashukuru wachezaji kwa moyo wa kupenda mchezo kujigarimia kuacha kazi zao kutoka mikoani ikiwa pamoja na wenyeji Dar es Salaam kuja kushiriki mashindano hayo ya Taifa  kwa kujilipia gharama zote za ushiriki hiyo inatia moyo sana kuwa ni dhahiri mnaopenda mchezo”.

Alisema Onditi michezo ni afya,michezo ni furaha na michezo ni kufahamiana basi aliwataka washiriki wote watumie nafasi hii ya kukutana katika kuyafanikisha haya yote.

Onditi alitoa wito kwa wafadhili kuwa wasiegemee kwenye mpira wa miguu tu kuna michezo mingi kama Darts na mingine wajitokeze wadhamini kwani kwa kutumia wapenda michezo kama hawa waliojitolea kutoka mikoani kwa gharama zao kuja kushiriki mashindano ya Taifa ni nafasi ya pekee  wewe mfanyabishara kutangaza biashara yako.

Mwisho aliwatakia mashiondano mema yenye amani kuwa waanze salama na wamalize salama na mwisho warejee majumbani salama salimini.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama alizitaja zawadi kuwa ni Vikombe na Pesa taslimu kwa mfumo wa mashindano utakaotumika ni wa Singles(mmoja mmoja), 

Doubles(wawili wawili) na Timu.

Mwisho Katibu wa Chama cha Darts Taifa, Kalley Mgonja aliitaja mikoa iliyofanikiwa kufika jijini Dar es Salaam kwa ushiriki wa mashindano ya Taifa kuwa ni Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha na wenyeji Dar es Salaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.