ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 8, 2023

WANAHABARI 6 WAKAMATWA KWA KUVUJA VIDEO INAYOMUONESHA RAIS AKIJIKOJOLEA.

 


Waandishi sita wa habari nchini Sudan Kusini wamekamatwa kwa kusambaza picha na video zinazomuonyesha Rais Salva Kiir akijikojolea. Katika video hiyo iliyosambaa mitandaoni, Rais Salva Kiir anaonyeshwa akijikojolea huku wimbo wa taifa ukipigwa.


  Katika video hiyo iliyosambaa mitandaoni mnamo Disemba 2022, Rais Kiir anaonyeshwa akijiendea haja ndogo huku wimbo wa taifa ukipigwa kwenye hafla. 

Kufuatia tukio hilo mashirika ya kutetea haki za vyombo vya habari yanasema kuwa wafanyakazi sita kutoka shirika la utangazaji la serikali walikamatwa wiki hii, BBC inaripoti. Hata hivyo, Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC) linasema video hiyo haikuonyeshwa kwenye kituo hicho. 


 Kulingana na Patrick Oyet ambaye ni rais wa Muungano wa Waandishi wa Habari wa Sudan Kusini, aliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba waandishi hao wanashukiwa kufahamu namna video hiyo ilivujwa.


 Waziri wa Habari wa Sudan Kusini Michael Makuei naye aliiambia Sauti ya Amerika kuwa watu wanapaswa kusubiri kujua sababu ya wanahabari hao kukamatwa. 


Sudan Kusini nchi mpya zaidi barani Afrika - mnamo 2011. Lakini nchi hiyo imekumbwa na mizozo mingi tangu wakati huo, ikivumilia migogoro ya kikatili, machafuko ya kisiasa, majanga ya asili na njaa. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.