Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye usiku wa Januari 7, 2023 alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo za umahiri wa Uandishi wa Habari (Tulia Trust Journalism Awards) 2022/23 iliyofanyika katika ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya.
Katika hafla hiyo ambayo lengo lake kuu ni kuchochea hamasa ya vyombo vya Habari pamoja na Wanahabari kufanya kazi zao katika weledi, ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, vyama vya siasa pamoja na Wananchi kutoka maeneo tofauti ambapo jumla ya shilingi milioni 22 zilitumika katika maandalizi ikiwemo zawadi.Joseph Mwaisango – Tuzo ya mshindi wa jumla (Online TV)
Baadhi ya Washindi walioibuka kidedea katika tuzo hizo kwa vipengele mbalimbali ni pamoja na ;-
i. Ezekiel Kamanga- Tuzo ya Uandishi wa Habari za madini na gesi (Online TV)
ii. Rashid Mkwinda- Tuzo ya Uandishi wa Habari za kilimo, mifugo na uvuvi (Online TV)
iii. Enock Simon – Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watoto (Online TV)
iv. Joseph Mwaisango – Tuzo ya mpiga picha bora (Online TV)
v. Joseph Mwaisango -Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Maliasili (Online TV)
vi. Kakuru Msimu – Tuzo ya Uandishi wa habari za utamaduni na michezo
vii. Joseph Mwaisango – Tuzo ya mshindi wa jumla (Online TV)
Kwa upande wa vituo vya redio
i. Washindi wa tuzo ya Uandishi wa Habari za afya ni Samwel Mussa, Pascal Ndambo na Fredrick Gumusu
ii. Washindi wa tuzo ya Uandishi wa Habari za mazingira ni Esther Lekasio na Joshua Sengo
iii. Washindi wa Habari za Michezo Jirani Mtembezi na Samwel Mussa
iv. Mshindi wa Habari za uchumi na biashara Prince Fungo
v. Mshindi wa tuzo ya Uandishi wa habari za unyanyasaji wa kijinsia ni Anitha Mahenge
vi. Mshindi wa Habari za Watoto ni Isakwisa Mbyale na Joshua Sengo
Wakati huohuo taasisi ya Tulia Trust ikiongozwa na Mkurugenzi wake Dkt. Tulia Ackson ilitoa mchango wa Shilingi milioni 15 kwa Umoja wa Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya (Mbeya Press Club Vikoba) kama sehemu ya kuwaongezea mtaji wa kukopeshana kwenye mfuko wao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.