ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 23, 2013

KANUNI MPYA ZA MAHAKAMA YA BIASHARA ZATAZAMIWA KUSAIDIA KUPUNGUZA MLUNDIKANO WA KESI


Mgeni rasmi Aishiel Nelson Sumari ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Mwanza akisoma maelezo ya ufunguzi wa semina ya Uhamasishaji kanuni mpya za Mahakama ya Biashara mkoani Mwanza iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.

Washiriki wa semina hiyo wakisikiliza kinachojiri.
Sheria hizo mpya zimekuja ili kuleta Ufanisi kwa jamii kwa kuharakisha kesi zilizo na migogoro ya kibiashara kwa kuokoa muda na jamii iweze kuendelea na shughuli nyingine za uzalishaji badala ya kushinda mahakamani kuzungushana na mashauri. 
Costantine Mutalemwa wakili wa kujitegemea akitoa mwongozo katika mada mbalimbali zilizowasilishwa kwenye semina ya Uhamasishaji kanuni mpya za Mahakama ya Biashara mkoani Mwanza iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya jiji la Mwanza
Kwa sasa ndani ya kanuni hizo mpya za uendeshaji mashauri ya kesi za madai yenye sura za kibiashara masuala ya kuahirisha kesi bila sababu za msingi hayatopewa nafasi kwani mahakimu watapaswa kulipia gharama za kuahirisha kesi wanapokuwa na sababu zao binafsi.
Washiriki wa semina hiyo pamoja na wawezeshaji wakisikiliza kinachojiri.
Changamoto ya kulazimika kuwa na vitendea kazi vya kiteknolojia kwa uchambuzi wa sheria na kuwasiliana na wateja wenye kesi imeibuka ndani ya semina hiyo kwani mawakili wanapokwenda kwenye kesi mahakama ya biashara watapaswa kuzifahamu vyema kesi zao wanazowakilisha na kuwa tayari kujibu maswali ya kesi husika iwapo mahakama itahitaji ufafanuzi.
Washiriki wa semina hiyo wakisikiliza kinachojiri.


Sehemu nyingine ya washiriki waliohudhuria semina ya Uhamasishaji kanuni mpya za Mahakama ya Biashara mkoani Mwanza iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.


Washiriki waliohudhuria semina ya Uhamasishaji kanuni mpya za Mahakama ya Biashara mkoani Mwanza iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya jiji la Mwanza wakipiga makofi kuashiria kuafiki moja kati ya mada za wawasilishaji wao.


Katika utangulizi Naibu msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania John Kahyoza  amesema kuwa lengo la mabadiliko hayo ya sheria za maamuzi mahakama ya biashara ni kuokoa muda wa jamii kwa kuhakikisha kesi zinamalizika kwa kipindi kifupi kuanzia mwezi mmoja hadi miezi 10, katika hilo muda huo ukipita na kama hakuna nyongeza inayokubalika kesi itatupwa.


Kwa umakiiii washiriki wa semina hiyo wakisikiliza kinachojiri.




Sikiliza mahojiano yangu na Mwanasheria......>
Jiografia ya kusanyiko la semina ya Uhamasishaji kanuni mpya za Mahakama ya Biashara mkoani Mwanza iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.