Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Symbion cha JK Yourth, na timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Lenox Musombo, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone. (Picha na Muhidin Sufiani)
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Symbion cha JK Yourth, na timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Zuberi Ada, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. (Picha na Muhidin Sufiani)
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Wakati Ujao Duce, Ezekiel Msuva ambaye ni mdogo wa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania,Simon Msuva, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. (Picha na Muhidin Sufiani)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (wa Nne kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo, Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Montage Ltd, Teddy Mapunda, wakipita kukagua timu za vijana za Academy, wakati wa Kliniki ya kuwahamasisha katika mchezo wa Soka katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. (Picha na Muhidin Sufiani)
MtotoHamis Kassim wa Kituo cha michezo cha Bom Bom, akionyesha umahiri wake wa kuchezea mpira wakati wa hafla hiyo ya Kliniki iliyoongozwa na mchezaji wa zamani wa timu ya Everton. Leon Osman. (Picha na Muhidin Sufiani)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone, wakati wa hafla hiyoiliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,leo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (kushoto) akimfurahia na kumpigia makofi,kijanaAbubakar Said wa Kituo cha michezo cha Wakati ujao wakati wa Kliniki iliyofanyika Uwanja wa Taifa,leo.
MSHINDI KOMBE LA SPORTPESA KUWAVAA EVERTON DAR JULAI 13
Na Mwandishi Wetu
SportPesa
imeanza kuthibitisha nia yake ya kendeleza soka la Tanzania kwa kutangaza kuwa
mshindi wa michuano ya SportPesa Super Cup atawavaa miamba wa soka wa
Uingereza, Everton. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya Ligi Kuu ya
England kucheza na klabu ya soka ya Afrika Mashariki.
Tangazo
hil limetolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa,
Pavel Slavkov, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas, Muu wa masoko
wa Kimataifa, Joyce Kibe, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton, Robert Elstone, Balozi
wa Everton FC, Leon Osman, Waziri wa Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Murugenzi
wa Michezo Yusuph Singo, Rais wa TFF Jamal Malinzi na wanahabari. Mechi hiyo
inayosubiriwa kwa hamu itapigwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
SportPesa
ilitangaza Mei 24 kwamba michuano ya SportPesa Super Cup itafanyika jijini Dar
es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru ikishirikisha timu nne (4) za Tanzania dhidi
ya timu nne (4) kutoka Kenya. Timu sita (6) kati yazitakazoshiriki michuano
hiyo ni klabu washirika rasmi wa SportPesa. Simba SC, Young Africans SC na
Singida United FC ni washirika wa SportPesa Tanzania wakati Nakuru All Stars,
AFC Leopards na Gor Mahia ni washirika wa SportPesa kutoka Kenya. Tusker FC ndiomabingwa
wa Ligi Kuu ya SportPesa ya Kenya wakati Jang’ombe Boys FC ni vinara katika
Ligi Kuu ya Zanzibar.
Akifurahia
ujuio wa Everton, Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Pavel Slavkov alisema; “Tunafuraha
kuwakaribisha Everton nchini Tanzania, ziara yao itakuwa na manufaa siyo tu kwa
klabu za hapa zitakazopata fursa ya kucheza na mabingwa hao mara 9 wa Ligi Kuu
ya England, bali pia na taifa zima kwa ujumla.
“Katika ziara hiyo
tutashirikiana kufanya shughuli kadhaa za kurudisha kwa jamii.
“Tanzania inapaswa kujiandaa
kupata uzoefu mkubwa kutokana na uwepo
wa Everton mjini hapa.”
Robert
Elstone, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton alisema: “Maandaizi ya mwanzo wa msimu
mpya ni kipindi muhimu sana kwetu kwani kwa kocha Ronald Koeman na benchi lake
la ufundi wakiwaandaa wachezaji kwa ajili ya msimu mkubwa ujao. Kuwa timu ya
kwanza ya Ligi Kuu ya England kuja kucheza Tanzania itakuwa ni sehemu muhimu ya
maandalizi hayo.
“Tunafungua
milango mipya na hatuna shaka kwamba tutapata marafiki na kuongeza mashabiki
wetu kkmataifa tutakapokuja Julai.
“Najua
Ronald Koeman na wachezaji wanajiandaa kuja kucheza mechi nzuri dhidi ya moja
ya klabu bora ya Afrika Mashariki.”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.