Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
******
Azimio la Arusha ni tamko rasmi la kisiasa lililokusiwa kuongoza Tanzania Kijamaa kadiri ya kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Neno Azimio linatokana na Mji wa Arusha na lilipitishwa tarehe 26-29 January 1967.
Tamko la Arusha lina sehemu tano, Yaani Itikadi ya Chama cha TANU, Siasa ya ujamaa, Siasa ya kujitegeea, Uanachama wa TANU na Azimio la Arusha.
Kiini chake ni hiki, Tumeonewa kiasi chakutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha na unyonge wetu ndio umetufanya tuonewe.
Lengo kuu la Azimio la Arusha ni kupinga unyonyaji, ubaguzi ili kuleta usawa ndani ya jamii.
Hili lilikuwa ni AZIMIO lenye misingi ya utu, na lengo kubwa la AZIMIO la ARUSHA ni kujitegemea, kiuchumi na si kisiasa peke yake na hasa kuwaondoa Waafrika katika mawazo ya kitumwa, kama Bob Marley alivyoimba, Emancipate yourself from mental slavery.
Kitendo cha JPM kufuta posho, safari za nje, wakubwa kupunguzwa nguvu ya ubabe, Mali za watumishi wa umma kuhakikiwa, kuzuia kusafirishwa kwa wanyama hai na madini nje ya nchi, kuchunguzwa kwa mchanga wa madini, kutoa elimu bure yote haya ni matendo yanayoendana na misingi ya Azimio lililotaka kuondoa ubaguzi, kuondoa matabaka ndani ya jamii, kudumisha utu, kuondoa unyonyaji ili tuweze kujitegemea kiuchumi.
Tumeanza kuheshimiana sasa. Ule msemo wa laki si pesa umekufa kabisa, zile kauli za unanijua Mimi nani hakuna tena. Haki ipo kwa wote ndani ya jamii.
Hauwezi kuyafanya hayo bila ya kuwa na uzalendo kama alionao Rais Magufuli. Naona kila dalili Rais Magufuli akiturudisha kulienzi na kulidumisha Azimio la Arusha lililoasisiwa na Mwalimu Nyerere
Na Emmanuel J. Shilatu
01/06/2017
0767488622
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.