Baadhi ya wananchi waliojitokeza kutembelea hifadhi hizo jana (Jumamosi), wameipongeza Serikali kwa ofa hiyo iliyowawezesha kushuhudia vivutio vya utalii.
Cecilia Magandila, mkazi wa Mto wa Mbu wilayani Monduli, amesema ameshuhudia vivutio vingi katika hifadhi ya Manyara ambavyo hakuwahi kuviona.
“Nimeona wanyama, chemchem za maji ya moto na mazingira mazuri ambayo sikuwahi kuyaona,” amesema.
Mpishi mkuu wa hoteli ya Serena Manyara, Gervas Mhina na wafanyakazi wenzake kwa nyakati tofauti wakiwa katika lango la kuingia Hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti wamesema uamuzi wa Serikali utasaidia kuwafanya Watanzania kupenda uhifadhi.
Mhina amesema ni jambo la aibu kwa watalii kutoka Ulaya kuja kutembelea hifadhi na Watanzania hata wanaoishi jirani, hawajawahi kuingia hifadhini kushuhudia vivutio vya utalii.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Manyara, Dk Noelia Myonga amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa ambao kwa siku mbili zaidi ya Watanzania 300 wametembelea hifadhi hiyo.
Myonga amesema kujitokeza kwa watu hao kutasaidia kujua umuhimu wa kutunza mazingira na kutembelea vivutio vya utalii.
Ofisa wa Idara ya Uhusiano ya Hifadhi ya Ngorongoro, Nickson Nyange amesema zaidi ya watalii 400 wametembelea hifadhi hiyo kwa siku mbili na hifadhi imeandaa waongoza watalii kusaidia wanaofika.
Nyange ametoa wito kwa Watanzania kutumia fursa ya ofa ya bure kutembelea hifadhi za Taifa ili kuona umuhimu wa kutunza mazingira na kujionea vivutio vya utalii
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.