Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrsai ya Kongo(DR CONGO) zimetiliana saini ya makubaliano katika ushirikiano wa kuboresha sekta ya ulinzi ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mahusiano mema yaliyopo baina ya Mataifa hayo.
Akizungumza jana baada ya zoezi la kusaini hati ya makubaliano Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanzania *Stergomena Tax* amesema kwamba zoezi la makubaliano limeanza baada mazungumzo ya kamati ya ushirikiano sekta ya ulinzi *JPC* ambapo kamati hiyo ikafikia makubaliano hayo.
Aidha amesema kwamba makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano wa kuimarisha sekta ya ulinzi ya Tanzania na DR Congo ili kuwa na mwambata wa wanajeshi yaani Tanzania kupokea wanajeshi kutoka DR Congo huku DR Congo ikipokea wanajeshi kutoka Tanzania kwa ajili yakukabiliana na vitendo vya uhalifu.
“Makubaliano haya yamelenga kuboresha maeneo mbalimbali katika sekta ya ulinzi ikiwemo kubadilishana taarifa za kiintelejensia,kufanya kwa pamoja mafunzo na mazoezi ya kijeshi na kitaalamu, kutembeleana ‘ kushirikiana katika masuala ya maafa,pia kushirikiana katika tiba wakati wa oparesheni mbalimbali” amesema Waziri Stergomena
Aidha ameongeza kuwa hakuna maendeleo bila amani hivyo Tanzania na DR Congo zinahitaji kuimarisha Biashara na vichocheo vingine akitolea mfano miundombinu ya barabara pamoja na bandari huku akisihi DR Congo kuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa DR Congo *Gilbert Kabanda Kurhenga* amesisitiza kuendeleza mahusiano mazuri kati ya Taifa lake na Tanzania huku akiwa na imani kuwa kupitia makubaliano hayo ya kuboresha sekta ya ulinzi itasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
” Leo ni siku ya furaha kukutana katika mkutano huu wa kusaini hati ya makubaliano ya kuimarisha sekta ya ulinzi kwa mataifa yetu ambayo yamekua kama ndugu kufuatia ushirikiano wetu wa muda mrefu, hivyo naimani tutaendeleza uhusiano wetu na tutaboresha sekta ya ulinzi pamoja na mambo mengine muhimu kwa mataifa yetu ” amesema Kurhenga
CHANZO: FULL SHANGWE BLOG
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.