Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Isupilo namna ambavyo watatua mgogoro huo wa ardhi
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Isupilo wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakati wa kutafuta njia ya kutatua mgogoro wa ardhi katika kijiji hicho
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Isupilo namna ambavyo watatua mgogoro huo wa ardhi
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wananchi wa Kijiji cha Isupilo wilaya
ya Iringa wamesema kuwa viongozi wa Kijiji hicho wamekuwa chanzo cha migogoro
ya ardhi baina ya wananchi na wawekezaji.
Wakizungumza kwenye mkutano wa
hadhara na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo walisema kuwa kumekuwa
na mgogoro ambao umedumu miaka mingi.
Walisema kuwa kutokana na kutokuwa na
uongozi imara kumesababisha familia ya Mzee Kivike kuuza ardhi ambayo imekuwa
inakariwa na kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na wananchi kwa
zaidi ya miaka kumi na tano.
Waliongeza kuwa mwekezaji Overland
aliponunua shamba kwenye familia ya Mzee Kivike amejiongezea eneo la mipaka la
hekari zaidi ya 250 ambayo kwa sasa ndio ambalo linaleta mgogoro na wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya
Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa atamwita mwekezaji Overland, viongozi
wa ardhi na viongozi wa Kijiji ili kuhakikisha wanatatua mgogoro huo.
Moyo alisema kuwa mgogoro huo wa
ardhi utatuliwa kwa njia ya amani kwa kuhakikisha kila mtu anapata haki yake
kwa mujibu wa sheria za ardhi zinavyosema .
Juliasi Mgeni ni mmoja ya wananchi wa Kijiji cha Isupilo alisema kuwa mwenyekiti wa Kijiji hicho Joakimu kisinini ndio chanzo cha migogoro ya ardhi.
Mgeni alisema kuwa mwenyekiti huyo
amejimilikisha ardhi ya wananchi kwa kutumia madaraka aliyokuwa nayo.
Alisema kuwa watu wa ardhi
wanachochea mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na mwekezaji kwa kutoa taarifa
tofauti tofauti kila mara.
Mgeni alisema kuwa hawaridhishwi na maamuzi ya ofisi ya ardhi ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa hivyo mkuu wa wilaya anaombwa kutatua mgogoro huo.
alimalizia kwa kusema shamba la
muwekezaji kampuni ya Overland linahekari 1262 huku hekari 953 hazina mgogoro
wowote na hekari 296 ndio zinamgogoro ambao kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha tuhuma
hizo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.