Baada ya kula kiapo katika uga wa Kasarani, Naibu Rais Rigathi Gachagua alipanda jukwaani kutoa hotuba yake ya kuapishwa.
Katika hotuba yake, Gachagua alichukua muda huo kumrushia makombora yasiyo ya moja kwa moja rais mstaafu Uhuru Kenyatta.
Bila kumung'unya maneno, naibu rais alimshutumu Uhuru kwa kuzorotesha uchumi wa nchi, ambao serikali mpya itakuwa na kibarua kigumu kuujenga. "Ukweli wa mambo ni kwamba tumerithi uchumi duni ambao unakaribibia kufifia.
Tuna kazi kubwa ya kuikomboa nchi hii na kuirejesha pale ambapo Kibaki aliiacha," alisema Gachagua. "Tunarithi Uchumu Uliooza" Alisema serikali ya Kenya Kwanza itajitahidi kurudisha uchumi wa nchi katika mkondo alioacha marehemu rais Mwai Kibaki.
"Ninataka kuwaambia Wakenya kwamba mko huru hatimaye.
Hamfai kuzungumza na kila mmoja wenu kupitia Whatsapp kwa kuogopa kurekodiwa na kuteswa na mashirika ya serikali," aliongeza. Wakati uo huo, Gachagua alimkumbusha Rais William Ruto kwamba safari iliyo mbele yake si rahisi.
Katika hotuba yake ya kwanza kama naibu wa rais, Gachagua alitoa wito kwa Wakenya kuombea utawala mpya huku ukijitahidi kurudisha uchumi katika mwelekeo wake.
Gachagua alibainisha kwamba kwao kuwa mamlakani ni kazi ya Mungu na maombi kutoka kwa Wakenya. "Haikuwezekana sisi kushinda uchaguzi huu ni kwa mkono wa Mungu leo mtoto kutoka familia maskini ameapishwa kuwa rais wa Kenya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.