Familia yake imejawa na furaha baada ya jamaa wao kurejea nyumbani wakisema kuwa alitoweka mwaka 1969.
Kwa mujibu wa familia yake, Njeru Mwiru ambaye amerejea akiwa na umri wa miaka 70, alitoweka akuwa kijana. Mwiru amefichua kuwa kwa miaka 53 ambayo hajakuwa nyumbani kwao amekuwa akiishi katika Kaunti ya Kitui.
Familia yake ilikuwa na furaha kubwa kumuona, ndugu zake wakisema kuwa hawakuwa wamechoka kumtafuta.
Mmoja wa ndugu zake wadogo alisema kuwa alikuwa amemtafuta eneo la Ukambani kufuatia ripoti kuwa Mwiru alikuwa anaishi eneo hilo. Katika muda wa miaka 53 ambao amekuwa ametoweka, Mwiru hakuoa wala kupata watoto.
Familia yake inasema kuwa alirejea nyumbani akiwema amebeba nguo zake katika gunia na upanga ambao alinunua akiwa mafichoni.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.