Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Meli mpya ya M.V Mwanza (Hapa kazi Tu) wakati wakimsikiliza Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria Meja Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia katika Sherehe za Uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuashiria uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria katika sherehe zilizofanyika eneo la
Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwachangia Kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza walipokuwa wakiimba kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019
Kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza walipokuwa wakiimba kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu),
Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Muonekano wa Chelezo inayojengwa katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai pamoja na viongozi wengine wakiinua mikono juu kwa umoja na furaha mara baada ya uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria katika sherehe zilizofanyika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba
08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkandarasi wa Ujenzi wa Meli mpya ya M.V Mwanza Bw. Dowan Kim kutoka kampuni ya STX Engine mara baada ya sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Desemba, 2019 ameweka jiwe la msingi katika miradi ya ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Chelezo na ukarabati wa meli za MV Victoria na MV Butiama katika Ziwa Victoria.
Sherehe za uwekaji jiwe la msingi katika miradi hiyo zimefanyika katika Bandari ya Mwanza Kusini Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wabunge, viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, viongozi wa taasisi mbalimbali, viongozi wa Dini na viongozi wa vyama vya siasa.
Ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu utakamilika Januari 2021 kwa gharama ya shilingi Bilioni 89.764 ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 43.74 na unatekelezwa na kampuni za ukandarasi za Gas Entec Company Limited na Kangnam Corporation za Jamhuri ya Korea kwa kushirikiana na Suma JKT. Kampuni hizi zimeshalipwa shilingi Bilioni 39.249.
MV Mwanza Hapa Kazi Tu itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari makubwa 3 na magari madogo 20, inatarajiwa kufanya kazi kati ya bandari za Mwanza, Kemondo, Bukoba na Musoma pamoja na kwenda nchi jirani za Kenya na Uganda na hivyo kukabiliana na adha ya usafiri kwa wananchi na mizigo katika Kanda ya Ziwa baada ya MV Bukoba kupata ajali ya kuzama majini mwaka 1996 na meli nyingine 4 kuharibika.
Ujenzi wa chelezo unafanywa na kampuni za STX Engine Company Ltd na Saekyung Construction Company Ltd, zote za Jamhuri ya Korea kwa gharama ya shilingi Bilioni 36.4 ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 68 na wakandarasi hao wameshalipwa shilingi Bilioni 32.85 sawa na asilimia 90 ya fedha zote.
Ukarabati mkubwa wa meli za MV Victoria na MV Butiama unafanywa na kampuni za KTMI Co. Ltd ya Jamhuri ya Korea na kampuni ya Yuko’s Enterprises (EA) Co. Ltd ya Tanzania kwa gharama ya shilingi Bilioni 27.71 ambapo mpaka sasa shilingi Bilioni 11.57 zimeshalipwa na kazi imefikia asilimia 65 na 60 mtawalia.
MV Victoria ina uwezo wa kuchukua abiria 1,200 na mizigo tani 200 wakati MV Butiama ina uwezo wa kuchukua abiria 200 na mizigo tani 100. Meli hizi zitakuwa zinafanya safari kati ya Bandari za Mwanza, Kemondo, Musoma, Bukoba na Nansio-Ukerewe.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Bw. Eric Benedict Hamissi amesema ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli hizo ambao unafanywa kwa kiwango cha kuzirudisha kuwa meli mpya kabisa unatarajiwa kukamilika Machi 2020.
Bw. Hamissi amempongeza na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa Serikali kufanya uwekezaji mkubwa wa mara moja ambao haujawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru, ambapo katika kipindi kifupi cha miaka minne imewekeza shilingi Bilioni 152 katika usafiri kwa njia ya maji, na ameahidi kuwa MSCL itafanya kazi kwa juhudi na maarifa kuhakikisha uchukuzi kwa njia ya maji unaboreshwa ukiwemo mpango mkakati wake wa kuanzisha huduma za usafirishaji mizigo katika Bahari ya Hindi kati ya Dar es Salaam, Comoro, Madagascar, Shelisheli na maeneo mengine.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa MSCL Bw. Hamissi kwa mageuzi makubwa anayoyasimamia ambayo yameonesha mwelekeo mzuri wa kampuni hiyo ya Serikali ambayo kwa kipindi kifupi imefufua meli nne kati ya 14 zilizoachwa na Hayati Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na amewapongeza wananchi wa Kanda ya Ziwa kwa kupata matumaini mapya ya kurejeshewa huduma za uhakika za usafiri kama alivyowaahidi wakati akiomba kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Amewapongeza Watanzania wote kwa kuchapa kazi na kulipa kodi zinazotumika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, na amesisitiza kuwa kutekelezwa kwa miradi hiyo ni uthibitisho kuwa Watanzania wanaweza hata bila kukopa au kupata ufadhili unaokuja na masharti magumu.
Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia fedha za Watanzania wenyewe ikiwemo mpango wa karibuni wa kujenga reli ya Mwanza – Isaka kwa kiwango cha kisasa (standard gauge), kukarabati meli nyingine 5 na ameahidi kuwa Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kununua meli mpya itakayofanyakazi katika Bahari ya Hindi kuanzia bajeti ijayo.
Amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Aloyce Kamwelwe kwa kazi nzuri zinazofanywa na wizara hiyo zikiwemo ujenzi wa meli 3 katika Ziwa Nyasa, ukarabati wa MV Liemba utakaofanyika hizi karibuni, uanzishaji wa Wakala wa Huduma za Bandari (TASAC) na upanuzi wa Bandari za Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Kemondo, Bukoba na Nyamilembe.
Kesho tarehe 09 Desemba, 2019 Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Mwanza
08 Desemba, 2019
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.