ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 4, 2023

SERIKALI YASEMA KILA MTOTO ANAYEZALIWA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO KUPIMWA USIKIVU WA MASIKIO BURE

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

1. Jeh ni magonjwa gani yanayojirudia kwa wagonjwa wengi wanaofika hospitalini hapo? 2. Hivi wajua kutoa nta kwenye masikio ni moja ya makosa tunayoyafanya bila kujua kuwa si salama kiafya na si sawa? 3. Licha ya wengine kuzaliwa na u-kiziwi na wengine kuupata ukubwani kutokana na mitindo ya maisha ikiwamo matumizi ya dawa bila kuwaona wataalamu, Jeh wajua kuwa unaweza kupata u-kiziwi kwa kurithi? ........................................................................................ ........................................................................................ HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO imeweka mkakati wa kukabiliana na tatizo la usikivu kwa kufanya upimaji kwa kila mtoto atakae zaliwa hospitalini hapo (New born hearing Screening), hivyo basi kila mtoto atakaezaliwa hospitalini hapa atapimwa uwezo wake wa kusikia kuanzia mwaka huu. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makiragi aliyemwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika hotuba yake aliyoisoma hii leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usikivu Duniani. TAKWIMU
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa mwaka 2020 ilipokea wagonjwa wenye changamoto ya usikivu 1635, kati yao asilimia 49.06% ni watu wazima (Kuazia miaka 18), asilimia 50.94% ni watoto. Kwa mwaka 2021 jumla ya wagonjwa walikua 856 kati yao asilimia 68.97% ni watu wazima, asilimia 31.03% ni watoto. Kwa mwaka 2022 jumla ya wagonjwa ni 970 kati yao asilimia 68.77% ni watu wazima na watoto ni asilimia 31.23 %. Takwimu zinaonesha ukubwa wa tatizo la usikivu wa masikio katika kanda na hata kitaifa. Juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanya na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ili kupambana na tatizo hilo, ikiwemo kuanzisha kitengo cha usikivu (Audiology Unit) hospitalini hapo mnamo mwaka 2016, na kuwapa matibabu ya kibingwa na kibingwa bobezi wagonjwa wanaofika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.