ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 4, 2023

HOSPITALI YA BUGANDO YAELEMEWA NA WAGONJWA WA NJE, YAJA NA MWAROBAINI WA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA YANUNUA MABASI MAWILI YA KISASA

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA "Wazo la kuanzisha klinini ya Madaktari Bingwa Bugando lilianza baada ya bodi ya uendeshaji ya hospitali kwa kushirikiana na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kufanya maboresho makubwa ya huduma za matibabu na kupelekea kuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa, hasa wagonjwa wa nje. Ambapo kwa sasa tunapokea takribani wagonjwa wa nje 810 kwa siku sawa na wagonjwa 24,000 kwa mwezi na lengo letu la mbeleni ni kupokea zaidi ya wagonjwa wa nje 30,000 kwa mwezi" amesema Dr. Fabian Massaga, Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Bugando, kisha akaongeza..... "Ongezeko hili la wagonjwa lilisababisha bodi ya uendeshaji wa Hospitali kupata wazo la kuanza kufungua matawi mbalimbali ili kupunguza msongamano wa wagonjwa ndani ya hospitali mama Bugando, ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa huduma za afya na kuzisogeza kwa ukaribu zaidi ili kuwafikia wananchi wote"

Muonekano wa jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.

Ukarabati, ununuzi wa mashine za kisasa, dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na uwekezaji mzima uliofanyika katika kliniki hiyo mpya ya 'Bugando Specialized Polyclinic' imegharimu takriban shilingi bilioni 2.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi akizindua moja ya mabasi mawili yaliyonunuliwa na Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwaajili ya wafanyakazi wake, hii ni mara baada ya kuzindua jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Dr. Fabian Massaga 'akipiga gia' kwa moja ya mabasi mawili yaliyonunuliwa na Hospitali hiyo kwaajili ya wafanyakazi wake, hii ni mara baada ya kuzindua jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.

Pozi la Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi mara baada ya kuzindua mabasi mawili yaliyonunuliwa na Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwaajili ya wafanyakazi wake, hii ni mara baada ya kuzindua jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.

Wawakilishi wafanyakazi Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando.

Mabasi mawili yaliyonunuliwa na Hospitali ya Rufaa ya Bugando , yaliyozinduliwa hii leo sanjari na kuzindua jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.