ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 1, 2023

KAMPENI YA SOMA NA MTI SAFARI YA UHAKIKA KUELEKEA TANZANIA YA KIJANI MWANZA.

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Shughuli nyingi zinazofanywa na binadamu kama uchomaji mkaa, uchomaji misitu, ukataji miti, uvunaji mbao usio na mpangilio vimechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira. Ni mwaka sasa tangu kuanzishwa kwa kampeni ya SOMA NA MTI iliyozinduliwa kitaifa jijini Dodoma mnamo Tarehe 20 mwezi January Mwaka jana 2022 chini ya mwasisi wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Selemani Said Jafo ikiwalenga wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo kote nchini kusimamia utunzaji wa mazingira, huku kila mwanafunzi akijivunia utunzaji na ukuzaji wa mti wake, lengo na Madhumuni ni kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kuifanya Tanzania kuwa ya kijani. Baada ya kampeni hiyo kupita mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Dodoma sasa kampeni hiyo imeingia jijini Mwanza ikianzia Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agustino almaarufu SAUTI ambapo wanafunzi wa chuo hicho wameungana na wanafunzi wa vyuo vingine kupanda miti kwenye mazingira ya chuoni hapo. Mhe. Hamisi Mamza Hamisi Chilo ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika tukio hilo. "Hapa nchini kuna takriban wanafunzi milioni 14.1 ambao kila mmoja akipanda mti wake itasaidia katika kukabiliana na changamoto hizo za kimazingira ikiwemo ukame na uhaba wa maji" alisema Mr Tree Vyuo vingine vilivyoshiriki zoezi hili ni pamoja na Bugando, City College, Tandabui, CBE, TTC Butimba, Mipango, BOT, IFM, VETA, TIA na kuchagizwa kwa njia ya elimu kupitia kituo cha redio Jembe Fm Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.