Mbegu mpya aina ya UKM 08 toka kampuni ya Quton, ikiwa kwenye sahani ya maonesho, mbegu hii tayari imefanyiwa majaribio na kuwa na sifa ya kuota bila kubahatisha nayo imekuja sokoni sasa kwaajili ya kuiondosha ile ya zamani iliyojulikana kama UKM 91 pamoja na ile ya manyoya.
Tanzania imekuwa ikipoteza mbegu nyingi sana wakati wa upandaji kutokana na matumizi ya mbegu hizi za manyoya ambazo hazijachambuliwa kubaini yapi ni makapi lakini sasa kuna mikakati ya kuziondosha mbegu hizi zisizochambuliwa na kuziingiza zile za uhakika.
Mbegu iliyochambuliwa aina ya UKM 08 ambayo haijawekwa dawa toka kampuni ya Quton, mbegu hii tayari imefanyiwa majaribio na kuwa na sifa ya kuota bila kubahatisha nayo imekuja sokoni sasa kwaajili ya kuiondosha ile ya zamani iliyojulikana kama UKM 91 pamoja na ile ya manyoya.
Meneja wa uzalishaji mbegu mpya toka kampuni ya Quton, Phineas Chikaura akitoa maelezo kwenye moja ya shamba darasa, ambalo ndilo wanalofanyia majaribio katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Waandishi wa habari wakichukuwa taswira za ukuaji wa mbegu zilizopandwa kwenye moja ya shamba darasa, ambalo ndilo wanalofanyia majaribio katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mtaalamu wa mbegu kiwanda cha Quton, Upendo Matulanya akitoa maelezo mbele ya waandishi wa habari juu ya uotaji na ukuaji wa mbegu mpya aina ya UKM 08 kwenye moja ya shamba darasa, ambalo ndilo wanalofanyia majaribio katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Hivi ndivyo mbegu aina ya UKM 08 inavyochipua katika shamba la majaribio.
Katika shamba hili mbegu aina mbalimbali zimepandwa kwaajili ya majaribio, kuanzia zile zenye manyoya, zile ambazo hazijapakwa dawa na mbegu mpya aina ya UKM 08.
Ndani ya chumba maalum cha kupandia mbegu toka kampuni ya Quton, na hapa ni majaribio ya uotaji wa mbegu aina ya UKM 08 ndani ya eneo la kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mtaalamu wa mbegu kiwanda cha Quton, Upendo Matulanya akitoa maelezo ndani ya chumba maalum cha kupandia mbegu toka kampuni ya Quton, juu ya majaribio ya uotaji wa mbegu aina ya UKM 08 ndani ya chumba hicho kilicho ndani ya eneo la kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mara baada ya kupata elimu ya shamba darasa safari ya waandishi wa habari ilielekea kwenye kiwanda cha uzalishaji pamba.
Meneja wa uzalishaji mbegu mpya toka kampuni ya Quton, Phineas Chikaura akitoa maelezo kwenye moja ya maghala ya kuhifadhi na kuchambua mbegu za pamba katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Wanahabari ndani ya katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Muonekano wa ndani kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mratibu mkuu wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea kiwanda cha uzalishaji mbegu toka kampuni ya Quton, Bw. Kyaruzi akiwa ndani ya katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Pamoja na uzalishaji wa mbegu za pamba zilizonyunyizwa dawa pia Kampuni ya Quton huzalisha mbegu zisizo na dawa kutokana na haki za kimazingira.
Mifuko ya mbegu za pamba katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Kiwanda cha Quton Tanzania Limited kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Msimamizi mkuu wa Kampuni ya uchambuzi wa mbegu za pamba Quton Tanzania Limited, Pradyumanshinh Chauhan, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
NA: ALBERT G. SENGO
SIMIYU
SERIKALI inatarajia kuondoa mbegu ya pamba aina ya UK 91 isiendelee kutumika katika uzalishaji wa zao la pamba kutokana na mbegu hiyo kushindwa kuzalisha pamba nyingi na yenye ubora.
Mkurugenzi wa bodi ya pamba Kanda ya Ziwa Jones Bwahama ametoa kauli hiyo wakati waandishi wa habari walipotembelea kiwanda cha kuzalisha mbegu ya pamba cha Quton wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Amesema kuwa hivi sasa bodi ya pamba kwa kushirikiana na wadau wa zao hilo wanajipanga kuongeza uzalishaji wa mbegu ya sasa inayofanya vyema kwenye kilimo aina ya UKM 08 ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2019 mbegu aina ya UK 91 iwe imeshaondoka kwenye mzunguko wa matumizi kwa wakulima. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Bwahama ameongeza kuwa mkakati wa bodi ya pamba ni kuhakikisha kuwa uzalishaji wa zao la pamba unaongezeka ikiwa ni sambamba na kasi ya kilimo cha mkataba.
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Phiniazi Kaula ni meneja wa mashamba ba ubora wa mbegu kutoka kampuni ya
QUTON anazungumzia hatua ambazo zinazochukuliwa kwaajili ya kuongeza uzalishaji wa mbegu aina ya UKM 08. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Mbegu iliyopo kwaajili ya uzalishaji wa zao la pamba imezalishwa mwaka 1990 na mbegu hiyo imekuwa haizalishi vya kutosha na kutoa pamba sawia kama vile inavyotakikana, jambo ambalo limechangia kudidimiza uzalishaji wa zao hilo na kuwafanya baadhi ya wakulima kukata tamaa ya kuzalisha zao hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.