HATIMAYE na baada ya mjadala mkubwa kuhusu matokeo
ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti, Tume Huru ya Uchaguzi na
Mipaka ya Kenya (IEBC) jana usiku ilimtangaza Uhuru Kenyatta kuwa ndiye
aliyeibuka na ushindi wa kiti cha rais wa nchi hiyo.
Matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa IEBC Bw. Wafula Chebukati yameonyesha kuwa Uhuru Kenyatta aliyegombea kwa tiketi ya chama cha Jubilee alipata ushindi baada ya kujizolea kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27 ya kura zote huku mshindani wake mkuu Raila Odinga wa muungano wa upinzani wa NASA akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74 ya kura zote.
Mwenyekiti wa IEBC Bw. Wafula Chebukati
Kwa matokeo hayo, Rais Uhuru Kenyatta wa mrengo wa Jubilee na Naibu wake William Ruto wataongoza tena Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Baada tu ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Kenya, mamia ya wafuasi wa chama cha NASA walimiminika mitaani wakiandamana kupinga matokeo hayo. Ripoti kutoka Nairobi zinaeleza kuwa polisi wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kudhibiti malalamiko ya kisiasa yaliyoibuka katika mji wa Kisumu magharibimwa Kenya iliko ngome kuu ya upinzani, eneo la mabanda la Mathare katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, Siaya, Homa Bay and Migori.
Raila
Odinga ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa Uhuru kenyatta katika uchaguzi
wa mwaka huu wa rais aligombea kiti hicho kwa mara ya kwanza katika
uchaguzi wa mwaka 1997 na hii ilikuwa mara ya nne kwa mwanasiasa huyo
kuchuana kwa ajili ya kuingia Ikulu ya Nairobi bila ya mafanikio. Katika
uchaguzi wa mwaka 2007 Raila Odinga na mrengo wake walidai kwamba,
kulifanyika udanganyifu mkubwa katika matokeo ya uchaguzi, suala mbalo
lilizusha machafuko makubwa kote nchini Kenya.
Zaidi ya watu 1200
waliuawa katika machafuko hayo na malaki ya wengine walilazimika kuwa
wakimbizi. Wakati huo Odinga aliwasilisha malalamiko mahakamani ingawa
mara hii NASA imesisitiza kuwa, haitaelekea mahakamani kukata rufaa na
hadi sasa haijulikani iwapo itabadilisha mawazo yake na kutaka haki
katika idara ya mahakama au la.
Akihutubia
mara baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa cheti cha kuchaguliwa,
Rais mteule Uhuru Kenyatta amewaomba Wakenya wadumishe amani na
kushirikiana na serikali yake kukuza taifa hilo. Vilevile amemshauri
kinara wa Nasa, Raila Odinga kwamba uchaguzi huo ulikuwa mashindano tu
na haufai kuleta chuki.
Matamshi
hayo ya Uhuru Kenyatta yanapata maana kwa kuzingatia muundo wa kikabila
wa siasa za Kenya ambao umekuwa na nafasi na ushawishi mkubwa katika
masuala muhimu kama chaguzi za rais Bunge la kadhalika.
Changamoto
nyingine kubwa ni maradhi ya malaria, virusi vya Ukimwi, kifua kikuu na
matatizo ya kichumi ambayo rais mteule Uhuru Kenyatta aliahidi
kukabiliana nayo katika kampeni zake za uchaguzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.