MUUNGANO wa upinzani wa NASA nchini Kenya
umetangaza kuwa utakubali matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika juzi kote
nchini humo iwapo utaruhusiwa kutazama data za asili katika sava za
kumputa za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya nchi hiyo (IEBC).
Hatua
hiyo inatathminiwa kuwa, ni ishara ya kulegeza msimamo wa muungano wa
upinzani ambao umekataa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya
IEBC na kutoa wito wa kutangazwa mgombea wake, Bwana Raila Odinga kuwa
ndiye mshindi wa uchaguzi wa Rais.
Wakala
wa uchaguzi wa muungano wa NASA, James Orengo amewaambia waandishi
habari mjini Nairobi kwamba, chama hicho kiko tayari kukubali matokeo ya
uchaguzi iwapo IEBC itafungua sava za komputa za matokeo ya uchaguzi na
kuruhusu NASA kutazama yaliyomo.
Awali
Bwana Musalia Mudavadi ambaye ni Wakala Mkuu wa NASA katika uchaguzi
huo amesema, vyanzo vyao vya siri ndani ya IEBC vimewapa ithibati kuwa
Odinga amepata kura zaidi ya milioni nane huku Rais Uhuru Kenyatta
aliyewania kiti hicho kwa muhula wa pili kupitia Chama cha Jubilee
akipata kura milioni saba na laki saba.
Kuna hofu ya kutokea ghasia nchini Kenya
Msimamo wa sasa wa NASA uliotangazwa na James Orengo unatambuliwa
kuwa ni aina fulani ya kulegeza kamba katika misimamo ya awali ya
muungano huo.
Murithi
Mutiga ambaye ni mwanachama wa kundi la International Crisis Group
amesema msimamo wa sasa wa NASA ni dalili na kulegeza msimamo.
Hadi
tunaingia mitamboni Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya ilikuwa
ikisubiriwa kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wakati wowote. Polisi na
askari usalama wamesambazwa katika maeneo yote muhimu ya jiji la Nairobi
kwa ajili ya kulinda usalama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.