NA VICTOR MASANGU,PWANI
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mbio za mwenge kitaifa utakaofanyika katika viwanja vya shirika la Elimu Kibaha Mkoani Pwani, Aprli 02,2025.
Hayo yamebaishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kutembelea na kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Mwenge wa uhuru ambapo ameridhishwa na maandalizi yalipofikia.
Alisema uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2025 utakuwa Aprli 02 katika viwanja vya shirika la elimu kibaha na kwamba mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa jamuuri ya muungano wa Tanzania Dk Philip Isdor Mpango.
Aidha alisema baada ya mbio hizo kuzinduliwa, mgeni huyo rasmi atawakabidhi viongozi sita wa mbio za mwenge walioandaliwa kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani jukumu la kukimbiza mwenge katika mikoa 31 yenye jumla ya halmashauri 195 kwa siku 195.
"Napenda kutoa taarifa kwa umma kuwa uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru utakuwa 02, Aprli,2025 katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha na mgeni rasmi atakuwa makamu wa Raisi wa Tanzania Dk. Phlip Isdory Mpango"alisena
Alisema mwenge wa uhuru utafanyakazi ya kuhamasisha amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa sambamba na kuhimiza wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo yao.
Alisema mwenge wa uhuru 2025 umebeba ujumbe "jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu" na kwamba umelenga kuwaelimisha na kuwakumbusha wananchi wote kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu.
"Sambamba na ujumbe huo pia umelenga kuwaelimisha wananchi kupambana na maradhi yanayotishia ustawi wa watu wetu Ikiwemo UKIMWI,malaria na kupambana na matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vya rushwa"alisema
Mbali na hilo amesema maandalizi yamekwisha kamilika kwa zaidi ya aslimia 90 ambapo ametoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa pwani na mkoa jirani kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amebainisha kwamba maandalizi kwa sasa yamefikia kiwango cha asilimia zipatazo 96 na kwamba hali ya ulinzi na usalama umeimarishwa kila kona.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.