NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Tabia ya baadhi ya wakuu wa taasisi na mashirika ya Serikali kupuuza mapendekezo ya wakaguzi wa ndani (Internal Auditors) imetajwa kuwa chanzo cha taasisi nyingi za Serikali kupata hati chafu kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kila mwaka. Tabia hiyo imebainishwa jana Jumatatu Machi 24, 2025 na rais wa Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani ya Kimataifa nchini Tanzania (IIA), Dk Zelia Njeza wakati wa uzinduzi wa mkutano wa wakaguzi wa ndani unaofanyika kwa siku tano kuanzia Marchi 24 hadi Machi 28, 2025. Dk Njeza ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania, amesema wakaguzi wa ndani wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, hata hivyo wamekuwa wakikumbana na vikwazo vya wakuu wa taasisi ama mashirika kutozingatia mapendekezo na ushauri.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.