NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) inaendeleza mkakati wake wa kutoa elimu kwa Umma kuhusu Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini kwa kuzungumza na waandishi wa habari waliopo jijini Mwanza. Akifungua semina ya siku moja ya waandishi wa habari jijini Mwanza Jumamosi, Machi 22, 2025 Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dkt. Emmanuel Mkilia amewapa Waandishi wa Habari mbinu bora za kuzingatia ili wafanye kazi kwenye Maadili na Misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini. Pia Dkt. Mkilia amejibu baadhi ya maswali muhimu yaliyoulizwa na waandishi wa habari ili yatumike kama msaada wa utoaji wa elimu kwa jamii. MASWALI 1. Jeh ni taasisi ngapi nchini Tanzania zinapaswa kujisajili, mpaka sasa taasisi ngapi zimejitokeza na hali iko vipi kwa mkoa wa Mwanza? 2. Mwisho wa kujisajili ni lini? 3. Kwanini watanzania wanapaswa kuwa na matumaini na Tume hii? 4. Jeh taasisi kubwa ni zipi na taasisi ndogo ni zipi? 5. Kwa ambao hawatakuwa wamejisajili baada ya muda wa usajili kupita ni adhabu gani watakazokutana nazo? 6. Tunaelekea katika duru za Uchaguzi Mkuu wa 2025 hapa nchini, nini rai yako kwa waandishi wa habari na wanasiasa katika kutimiza wajibu wao? 7. Jeh taasisi zinajisajili wapi na vipi? Mhandisi Stephen Wangwe ni Mkurugenzi wa usajili na uzingatiaji PDPC anatoa majibu. ........................................................................................................................ “Ili kuhakikisha kuwa mnazingatia maadili na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni muhimu kuzingatia mbinu bora zikowemo kujiridhisha na vyanzo vya habari kabla ya kuchapisha taarifa inayohusu mtu binafsi, hakikisheni kuwa chanzo ni sahihi na kinazingatia Sheria. Pia tumieni mifumo salama ya kuhifadhi na kusambaza taarifa ili kuhakikisha kuwa taarifa za watu hazivuji” amesema Dkt. Mkilia Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini, ilianzishwa rasmi tarehe 01 Mei, 2023 kufuatia kupitishwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11, 2022.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.