VICTOR MASANGU PWANI
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge amezindua Mradi wa kilimo cha Pamba Wilayani Rufiji utakaotekelezwa na Kampuni ya Rufiji Cotton Ltd ambapo uzinduzi huo umeambatana na kupokea matrekta na pikipiki zitazotumika kwenye mradi huo.
Akizungumza na Wanachi wa Rufiji wakati wa hafla hiyo, Mhe Kunenge amewapongeza wawekezaji hao kutoka India kwa uwekezaji huo amesema hana shaka na mwekezaji huyo kwa sababu ni mzoefu kwenye sekta ya Pamba.
Kunenge amesema kuwa kwenye historia Pamba ilianza kulimwa Nchini kwa mara ya kwanza wilayani Rufiji mwaka 1964 Amesema kuwa Serikali ipo tayari kuumpa ushirikiano mwekezaji na kimtaka mwekezaji Afanye yote aliyoahidi.
Ameeleza Kupitia uwekezaji huo vijana watapata ajira, Kodi kwa serikali na ujuzi. Ameeleza kuwa kwenye kipaumbele chake kwa Mkoa wa Pwani Kilimo ni kipaumbele na bado hakijafanya vizuri.
Pia amepongeza wilaya ya Rufiji kwa kuendelea kuwapokea wawekezaji kwa sasa wilaya hiyo ina wawekezaji wakubwa wa Kilimo cha Sukari, na Kilimo cha Pamba. Kunenge amewataka wakazi wa Rufiji kutumia fursa hizi walizopata. Amewapongeza wakazi wa chumbi kwa kuwezesha uwekezaji huo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Bw. Wille Mtunga ameeleza kuwa ziara ya India ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imezaa matunda na leo tunazindua mradi wa Pamba Rufiji.
Alisema kuwa ili kuwa na kilimo bora wameleta timu ya ushindi ambao ni maafisa ugani 24 watakao hudumu kwenye vijiji hivyo 24. ameeleza kuwa Mpaka sasa wamesajili wakulima wenye jumla ya Hekari 3012 wilayani Rufiji.
Naye Balozi wa zao la Pamba Nchini Mhe Aggrey Mwanri, ametuma Salaam kwa Mhe Rais Dkt Samia za pongezi kwa kuvutia uwekezaji katika sekta ya Pamba.
Ameeleza kuwa kazi yake kama balozi ni kufanya pamba ipendeke kwa wananchi wote. Ameeleza wamechukua takwimu za wananchi wote wa Rufiji waliotayari kulima Pamba.
Ameeleza kuwa Kilo zinazozalishwa wilayani Rufiji ni laki moja na kiwanda kitakacho jengwa kitahitahi kilo laki tano. Ameeleza kuwa Halmshauri hiyo ikilima pamba vizur itapata ruzuku amehamasisha vijana wote kulima pamba na wale maafisa ugan 24 walioajiriwa kuhakikisha wanafanya kazi iliyokusudiwa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Rufiji Cotton Ltd Bw Hassan Kinje ameeleza kuwa wamekuja kuwekeza Rufiji kwa sababu ya Mazingira mazuri ya uwekezaji, ameeleza kuwa wamekuja kulima Rufiji na si Kununua Pamba. Ameeleza kuwa kampuni hiyo itatoa uwezeshaji wa huduma bure ya matrekta kwa ajili ya kilimo.
Aidha wameajiri maafisa ugani 24 na kutoa pikipiki ambazo zitatumika kutoa elimu kwa wakulima. Ameeleza kuwa wanategemea kujenga kiwanda cha kuchambua Pamba, kiwanda vya nguo. Wamepongeza ushirikiano mkubwa walioupata kutoka katika uongozi wa Mkoa katika kufanikisha uwekezaji huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.