NA ALBERT G.SENGO/MWANZA Hatimaye Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imezindua rasmi jarida maalum linaloangazia jitihada endelevu za kudhibiti uoto vamizi wa gugumaji katika Ziwa Victoria. Uzinduzi huo umefanyika Mei 13/2025 katika viwanja vya Ofisi za Bonde vilizopo kata ya Igogo wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wahudumu na wafanyakazi wa shughuli za bonde kutoka serikalini, mashirika ya mazingira, na jamii zinazozunguka ziwa Victoria. Licha ya kuipongeza Bodi kwa hatua hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameiagiza kuhakikisha Jarida waliloliandaa kuhusu kukabiliana na uvamizi wa Gugumaji jipya aina ya Salvinia Molesta, linawekwa katika mifumo mbalimbali ili jamii iweze kuona, kusoma na kusikiliza ili kupata elimu tosha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.