ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 4, 2011

BREAKING NEWS: MAJAMBAZI WATANO WENYE SILAHA WAUAWA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA

Mafisa wa jeshi la polisi katika tukio.
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwaua majambazi watano waliokuwa na silaha hatari za moto wakiwa katika harakati za kufanya uporaji kwenye moja ya maduka ya vifaa vya ujenzi yaliyopo mtaa wa Nyerere jijini Mwanza.Mtaa wa Liberty
Tukio hilo lilitokea Leo majira ya saa 3:30 asubuhi, katika duka la uuzaji wa vifaa vya ujenzi la mfanyabiashara mtanzania mwenye asili ya kiasia aliyejulikana kwa jina moja tu la Mukesh.

Majambazi hayo yaliyokuwa na silaha yalipovamia duka hilo na kukuta kiasi kidogo cha fedha cha shilingi elfu sitini ikiwa ni tofauti na matarajio yao (kukuta kiasi kikubwa cha fedha), yalishikwa na taharuki na kuanza mabishano kiasi cha kutoa mwanya kwa jeshi la polisi kuzunguka eneo la tukio na kuanza mapambano.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Liberatus Barow amesema kuwa mapambano hayo ya silaha yaliyodumu kwa muda wa dakika kumi jeshi lake limefanikiwa kuwauwa majambazi wote watano huku ikiripotiwa kuwa hakuna mwananchi yeyote aliyepoteza maisha.
Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la tukio.
Taarifa zinasema kuwa majambazi mawili kati ya matano yaliyouawa yamejulikana mmoja akiwa raia wa Burundi na mwingine akijulikana kwa jina la Maulid Said raia wa Tanzania.

Maulid Said ambaye ni jambazi sugu anahusishwa na matukio mbalimbali kanda ya ziwa likiwemo lile la mwaka 2009 lililotokea mtaa wa Liberty na kisha baadaye Nyegezi katika gesti ya Pambazuko ambapo jambazi hilo lilimpa majeraha ya risasi Koplo Shahban na kutokomea kusikojulikana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.