Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) wakisaini Mkataba wa Makubaliano
ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na
TADB.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto)
akimuangalia Mkuu
wa Huduma za Kisheria wa TADB, Bibi Neema Christina John (Katikati)
wakati akiendelea na zoezi la ugongaji wa mihuri Mikataba ya Makubaliano
ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na
TADB.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano (Kushoto) akibadilishana Mkataba wa Makubaliano
ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na
TADB
na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia).
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (Katikati) akizungumza na
Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kulia). Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi
Rosebud Kurwijila (Kushoto).
TANZANIA YA VIWANDA: BENKI
YA MAENDELEO YA KILIMO KUSAIDIA AZMA YA SERIKALI
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia
azma ya serikali katika kujenga Tanzania ya viwanda kwa kusaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda nchini kwa kutoa mikopo nafuu kwa wakulima
nchini.
Azma hiyo imetolewa na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila wakati wa utiaji saini Mkataba wa Makubaliano
ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na Benki hiyo katika hafla iliyofanyika Ofini
kwa Msajili
wa Hazina jijini Dar es Salaam.
Bibi Kurwijila amesema kwamba TADB itakeleza kwa vitendo
juhudi
za Serikali za Kujenga Uchumi wa Viwanda kwa kuhuisha uwekezaji kwenye
Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa
mazao ya Kilimo, mifugo, samaki na misitu ili kuongeza tija ya kilimo
hivyo kutoa malighafi kwa viwanda nchini.
“Benki
imepitia upya mpango mkakati wake katika kutoa mikopo ili kuwezesha
kufikia wakopaji wengi zaidi ili kuweza kufikia lengo la kuleta
maendeleo katika sekta ya kilimo hasa katika kuongeza tija ya kilimo
hivyo kutoa malighafi kwa viwanda nchini,” alisema
Bibi Kurwijila.
Bibi
Kurwijila ameongeza kuwa katika kuchagiza malengo hayo, TADB imejpanga
katika Kushirikiana na wadau
mbalimbali kufanya upembuzi wa miradi ya Maendeleo ya Kilimo na
Umwagiliaji nchi nzima ili kubaini mahitaji halisi ya fedha na pia
kusaidi kupanga maeneo ya vipaumbele ili kuanza kutoa mikopo hasa kwa
utaratibu mahsusi.
Ametaja
malengo mengine ya kimkakati ya TADB ni pamoja na kuboresha huduma kwa
kuanzisha mazao maalum
ya huduma za kibenki kwa wakulima wadogowadogo kulingana na mnyororo
husika wa thamani na pia kuanza huduma za Zaidi kupitia taasisi za fedha
zilizopo (wholesale lending and Refinancing) ili kufikia wakulima wengi
zaidi.
Kwa upande wake
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa mpaka sasa Benki imefanikiwa
kukopesha jumla ya shilling bilioni 6.5 kwa vikundi 20 vyenye jumla ya wakulima 2575.
Bw.
Assenga ameongeza kuwa Benki imeweza kuvijengea uwezo vikundi 336 vya
wakulima wadogowadogo vyenye jumla wa wanachama 44,400 katika mikoa ya
Iringa, Morogoro na Tanga.
“Kupitia
mafunzo hayo TADB imewezesha jumla ya vikundi 19 kutimiza masharti na
maandalizi ya msingi ya kuweza kukopa; Vikundi vingine vilivyobaki
vinaendelea kupatiwa
mafunzo ili viweze kufikia hali ya kuweza kukopesheka,” ameongeza.
Kwa
mujibu wa Bw. Assenga, TADB imeweza kuinua idadi ya wakulima watumiao
mabenki na vyombo vya fedha wapatao 2,359 ambao kati yao wanawake ni 863
sawa na asilimia 36.6
ya wanufaika.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo, Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano alisema
taasisi za umma zina wajibu wa kuisaidia utekelezaji wa mipango
mbalimbali ya Serikali ili kuleta maendeleo endelevu nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.