Vyombo vya usalama vya Kenya vimetahadharisha juu ya uwezekano wa kufanyika mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
George Kinoti Msemaji wa Polisi ya Kenya alisema jana usiku
kuwa tayari kumesambazwa taarifa kwamba magaidi tisa wanafanya kila
linalowezekana kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini humo.Magaidi wamekuwa wakifanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya serikali huko Kenya baada ya kupata pigo mbele wanajeshi wa Kenya. Kundi la kigaidi la al Shabab lenye makao yake Somalia limekuwa likifanya mashambulizi na hujuma mbalimbali katika ardhi ya Kenya; jambo linalowatia wasiwasi viongozi wa serikali ya Kenya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.