NA ALBERT G.SENGO/DODOMA
Kutana na Mhandisi Imelda Salum ambaye ni Mkurugenzi wa TCRA Kanda ya Ziwa akizungumza juu ya wajibu wa vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu 2025. Mhandisi Imelda ameyasema hayo akiwa katika Mkutano wa siku mbili wa wadau wa habari na TCRA, mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ukishirikisha Vituo vya utangazaji, waandaaji na wasambazaji wa maudhui mtandaoni, wauzaji wa vifaa vya utangazaji na wadau wote wa sekta ya utangazaji ukiongozwa na kauli mbiu 'Wajibu wa vyombo vya utangazaji kuelekea uchaguzi mkuu 2025'.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.