ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 23, 2018

LUGOLA - ASKARI ATAKAYESHIKWA NDEVU NA JAMBAZI KUKIONA





GSENGOtV
Ziara ya Waziri Kangi Lugola jijini hapa imekuja mara baada ya tukio kubwa la kusisimua lililotokea hivi karibuni baada ya jeshi la polisi mkoani Mwanza kufanikiwa kuanza kuvunja mtandao wa majambazi  ambapo mara baada ya kuzuka majibizano ya silaha za moto kwa zaidi ya muda wa dakika 45, polisi walifanikiwa kuwauwa zaidi ya majambazi 7 wanaosadikika kuhusishwa na matukio kadhaa ya uhalifu Kanda ya Ziwa. 
Akizungumza na maofisa wa polisi na baadhi ya askari wa vikosi vyote vya polisi jijini hapa leo Ijumaa Novemba 23,2018 katika viwanja vya polisi Mabatini, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema askari wote walioshiriki katika mapambano na kufanikisha zoezi hilo lililotokea Novemba 15, 2018 jijini Mwanza watapandishwa vyeo.
"Kwenye sheria yetu ya Jeshi la polisi na polisi wasaidizi sura ya 322, ukienda kwenye makosa ya kinidhamu ya askari, Ni kosa kwa askari kuwa mwoga, 'askari hupaswi kukimbia tukio' lazima ukabiloane nalo" Naomba nikuhakikishie Kamanda Shanna, kwa wale vijana wote waliofanya kazi kubwa kwenye tukio la juzi kukabiliana na majambazi, mimi kama Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi kwa amri ya Serikali tutawapa zawadi ya kuwapandisha vyeo" 
Lugola ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi kuwa wapo salama na kuwatumia salamu wanaofanya uhalifu kwamba bora wajisalimishe na kuacha mara moja vitendo hivyo vinginevyo watashughulikiwa popote watakapokuwa hata kama ni mapangoni maana Serikali ina mkono mrefu.
Awali, Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana amesema mkoa huo upo shwari licha ya kuwapo matukio kadhaa ya wahalifu lakini wamekuwa wakiwadhibiti kabla ya kutekeleza azma yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.